The House of Favourite Newspapers

Hapi Asema Serikali Itawakopesha Vijana Pikipiki

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi.

MKUUS wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi.  ametangaza na kutoa agizo kwa viongozi wa Halmashauri ya Kinondoni kuanza kutoa mikopo ya vitendea-kazi kwa vijana mbalimbali wilayani huo zikiwemo pikipiki ili vijana waweze kujikwamua kiuchumi.

 

Hapi amesema hayo alipowatembelea wafanyabiashara wa Soko la Ndizi ambao wanategemewa hivi karibuni  kuhamishiwa katika eneo la Kigogo Dampo.  Akizungumza nao alisema kuwa zipo fedha zaidi ya Sh. bilioni moja kwa ajili ya mikopo kwa vikundi vya vijana na kina mama ambazo zimekuwa hazitoki kwa kuwa watu wamekuwa hawataki kijiunga katika vikundi na kwenda kukopa.

 

“Vijana wanaotaka kukopa pikipiki waje wajiorodheshe wakopeshwe pikipiki walete rejesho serikalini.  Tuna billioni moja imekaa tu pale, eti tunasubiri vijana waje, watakuja lini? Sasa nataka kuona vijana wananufaika na fedha hizo wajikwamue ili familia zao nazo zinufaike.

 

“Nataka tuwakopeshe watu vitu ambavyo vinawasaidia moja kwa moja, tunataka tuwakopeshe watu dhana za kufanyia kazi,  nimeshaanza kumwambia mkurugenzi jambo hilo walifanye. Namwambia naibu meya kwamba wakijitokeza vijana 400 Kinondoni tukawakopesha pikipiki, nataka nikuhakikishie ndani ya muda mfupi fedha zile zinarudi.  Mpe mtu pikipiki chukua kadi itunze yeye analeta marejesho kila wiki una uhakika hapo wa kupata fedha iliyokopeshwa,” alisisitiza Hapi.

Comments are closed.