The House of Favourite Newspapers

SERIKALI KUPOKEA TRILIONI 1.8 KUTOKA BENKI YA DUNIA – Video

Serikali ya Tanzania imesaini Mkataba wa Makubaliano na Benki ya Dunia kupokea mkopo wa Tsh. Trilioni 1.8 wenye masharti nafuu unaoweza kulipwa ndani ya miaka 40 ambapo Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James amesema katika fedha hizo Tsh. Trilioni 1.04 zitaelekezwa katika Sekta ya Nishati na Tsh. Bilioni 800 katika Sekta ya Maji.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo baada ya makubaliano hao amesema Wizara ya Maji imejipanga kuhakikisha fedha hizo zinatumika ipasavyo.

 

Aidha, Wananchi katika vijiji takribani 17, watu 2,500,000 watapata huduma ya maji safi ya kunywa, 4,000,000 huduma ya usafi wa mazingira na vijiji 1250 vitanufaika na maji safi na salama.

SHUHUDIA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.