Serikali Kutumia Ndege Kuua Nzige Simajiro, Longido

Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda amesema ndege itapuliza sumu kuua nzige katika Wilaya za Simanjiro na Longido leo. Amewataka Wananchi kutookota au kula nzige waliokufa katika maeneo hayo.

 

 

Asema nzige wote watadhibitiwa na Wataalamu waliopo kwenye maeneo yenye dalili za uwepo wa wadudu hao hivyo Wananchi wasiwe na hofu.

 

Aidha, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Jumaa Mhina ameagiza Shule zote za Msingi na Sekondari kwenye maeneo yatakayopuliziwa viuatilifu kusitisha masomo kwa siku nne kuanzia leo.

Toa comment