The House of Favourite Newspapers

Serikali ya Iran Yawanyonga Majasusi Wanne Wanaodaiwa Kutumwa na Israel

0

Serikali ya Iran imewanyonga majasusi wa nne wa Israel waliohukumiwa kifo baada ya kukamatwa, wakituhumiwa kutumwa na Israel kuipeleleza nchi hiyo

Taarifa zilizotolewa na Shirika la Utangazaji la Iran, IRNA, imesema hukumu hiyo imetekelezwa leo Jumapili huku majasusi wengine watatu wakihukumiwa vifungo virefu gerezani.

IRNA imeeleza kuwa majasusi hao, walikamatwa na maafisa wa Jeshi la Revolutionary Guard ambapo baada ya upelelezi wa kina, walikutwa na hatia ya kujaribu kuvuruga amani nchini Iran, huku wakitajwa kutumwa na Shirika la Ujasusi la Israel, Mossad.

Shirika hilo limewataja walionyongw kuwa ni Hossein Ordoukhanzadeh, Shahin Imani Mahmoudabadi, Milad Ashrafi na Manouchehr Shahbandi.

Serikali ya Iran imekuwa ikiwakamata na kuwahukumu majasusi mbalimbali wanaokamatwa kwenye ardhi ya nchi hiyo, hususan kutoka kwa mahasimu wake wakubwa, Israel na Marekani.

Leave A Reply