The House of Favourite Newspapers

Serikali Yaanika Mikakati ya Kutangaza Hifadhi ya Taifa Katavi

0

SERIKALI kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema kuwa imekuwa ikitekeleza mikakati mbalimbali ya kuitangaza Hifadhi ya Taifa ya Katavi ili iweze kupata watalii wengi na kuongeza mapato.

 

Akizungumza jana Bungeni Jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Mary Masanja wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Martha Festo lililokuwa likihoji kuwa Serikali ina mpango gani wa kuitangaza Hifadhi ya Taifa ya Katavi, amesema serikali kwa kushirikiana na viongozi wa Mkoa wa Katavi waliandaa mpango mkakati wa kukuza Utalii katika mkoa huo mwaka 2019 na umesaidia kwa kiwango kikubwa kuitangaza hifadhi hiyo.

 

Amesema Hifadhi hiyo imekuwa ikitangaza Vivutio vya Utalii kupitia Vyombo mbalimbali vya habari vya ndani ya nchi na nje ya nchi ikiwemo mitandao ya kijamii kwa kuwa ni miongoni mwa Hifadhi zenye viboko,simba na twiga weupe.

 

Kwa upande wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Damasi Ndumbaro amesema serikali ina mpango mkakati wa kushirikiana na Halmashauri zote, Serikali za mitaa na Wilaya kuutangaza utalii ikiwemo kuwatumia wabunge kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika maeneo yao.

 

Leave A Reply