The House of Favourite Newspapers

Serikali Yafungulia Magazeti ya Mwanahalisi, Mawio, Mseto na Tanzania Daima

0

SERIKALI imeyafungulia rasmi magazeti manne ambayo ni Mwanahalisi, Mawio, Mseto na Tanzania Daima yaliyokuwa yamefungiwa kwa muda mrefu.

 

Uamuzi huo umetangazwa leo Alhamisi, Februari 10, 2022 na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari na kutoa leseni ya magazeti hayo.

 

Nape amesema “Agizo la Rais ni sheria na inapaswa kutekelezwa, leo nitatoa leseni kwa magazeti manne yaliyokuwa yamefungiwa ambayo ni Mwanahalisi, Mawio, Mseto na Tanzania Daima kwasababu ni vizuri kuondoka kwenye maneno tufanye vitendo hivyo tuanze na ukurasa upya sasa mwenye maneno yake aseme mwenyewe, kifungo kimetosha kikubwa kazi iendelee.” amesema Nape.

 

Uamuzi wa kufungulia magazeti hayo ni kutekeleza maagizo ya Rais Samia aliyoyatoa Aprili 6, 2021 wakati akihutubia na kusema vyombo vya habari vilivyofungiwa, viongozi wa Serikali wenye dhamana waangalie namna ya kuvifungulia ili vifanye shughuli zake kwa kuzingatia sheria za nchi.

 

Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile akimwomba Waziri wa Habari, Nape Nnauye kuyafungulia magazeti yaliyofungiwa ya MwanaHALISI, Tanzania Daima, Mseto na Mawio, “Rais aliagiza vyombo vilivyofungiwa vifunguliwe. Tunakuomba sana, heshima ya Tanzania imeharibika, tuvifungulie.” 

Leave A Reply