The House of Favourite Newspapers

Serikali Yapokea Gawio La Shilingi Bilioni 17 Kutoka Benki Ya CRDB

0
Waziri wa Fedha, Dkt. Philip Mpango akipokea mfano wa hundi ya gawio la shilingi bilioni 9.3 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki yah CRDB, Dkt. Ally Laay (watatu kushoto) kutokana na uwekezaji wa Serikali ndani ya benki hiyo kupitia Mfuko wa Uwekezaji wa DANIDA kwa kushirikiana na Serikali ya Denmark. Waziri Mpango Agosti 10, 2020 amepokea jumla ya gawio la shilingi bilioni 17 kutoka Benki ya CRDB ikiwa ni gawio kutokana na uwekezaji wa Serikali kuu, taasisi na mashirika yake. Wengine pichani ni Waziri wa TAMISEMI, Suleiman Jaffo (wanne kushoto), Waziri wa Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (watatu kulia), Balozi wa Denmark Nchini, Mette Dissing-Spandet (wapili kulia), Msajili wa Hazina, Athman Mbuttuka (wakwanza kulia), Makamu Mwenyekiti wa Bodi Benki ya CRDB, Prof. Neema Mori (wakwanza kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
 

BENKI ya CRDB Agosti 10, 2020 wamekabidhi jumla ya gawio la shilingi bilioni 17 kwa Waziri wa Fedha, Dkt. Philip Mpango ikiwa ni gawio kwa Serikali kuu, taasisi na mashirika yake kutokana na uwekezaji ndani ya benki yetu.

Mwaka huu tumetoa jumla ya gawio la shilingi bilioni 44.4 kwa Wanahisa wetu baada ya kupata faida ya shilingi bilioni 120.1 mwaka 2019 ikiwa ni ongezeko la asilimia 87 kulinganisha na faida ya shilingi bilioni 64 mwaka 2018.

Waziri wa Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (wapili kulia) akipokea gawio la shilingi bilioni 5.8 kutoka Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay (wapili kushoto) na kumkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF, Hosea Kashimba (wakwanza kulia), kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela. Benki ya CRDB imekabidhi jumla ya gawio la shilingi bilioni 17 kutokana na uwekezaji wa Serikali kuu, taasisi na mashirika yake.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI) Selemani Jafo akipokea gawio kutokana na uwekezaji wa Halmashauri za Mbinga, Lindi, Shinyanga, Mufindi, Chunya na Rungwe  jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Dkt. Philip Mpango akitoa hotuba yake katika hafla fupi ya kupokea jumla ya gawio la shilingi bilioni 17 kutoka Benki ya CRDB ikiwa ni gawio kutokana na uwekezaji wa Serikali kuu, taasisi na mashirika yake, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma leo.
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akisisitiza jambo wakati wa hafla fupi ya kupokea jumla ya gawio la shilingi bilioni 17 kutoka Benki ya CRDB ikiwa ni gawio kutokana na uwekezaji wa Serikali kuu, taasisi na mashirika yake, iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI) Selemani Jafo akizungumza wakati wa hafla fupi ya kupokea jumla ya gawio la shilingi bilioni 17 kutoka Benki ya CRDB ikiwa ni gawio kutokana na uwekezaji wa Serikali kuu, taasisi na mashirika yake, iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma.

 

Leave A Reply