The House of Favourite Newspapers

Kesi ya Idris, Mwenzake Yakwama Kortini

0

KESI  inayomkabili mchekeshaji maarufu nchini, Idris Sultan, na mwenzake, Innocent Maiga, imeshindwa kuendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumanne, Agosti 11, 2020, kutokana na wakili anayemtetea mshitakiwa, Elia Lioba,  kutokuwepo mahakamani.

 

Imeelezwa mahakamani hapo kuwa, Lioba amepata msiba, hivyo hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Yusto Ruboroga, ameiahirisha kesi hiyo mpaka Agosti 24, mwaka huu itakapoendelea na ushahidi.

 

Katika kesi hiyo iliyokuwa imekuja kwa ajili ya kuanza kutolewa ushahidi, Idris anakabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la kushindwa kufanya usajili wa laini ya simu ambayo ilikuwa inamilikiwa na mtu mwingine, kinyume cha sheria.

 

Mshitakiwa mwingine katika kesi hiyo ni mfanyabiashara Inocent Maiga anayekabiliwa na kosa la kushindwa kutoa taarifa ya mabadiliko ya umiliki wa laini ya simu hiyo.

Leave A Reply