The House of Favourite Newspapers

Serikali Yastuka Laini za Simu Zinavyotumika Katika Matukio ya Uhalifu

0

 

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dr.Faustine Ndugulile amewasihi Watumiaji wa simu kuangalia laini zilizosajiliwa kwa majina yao kupitia *106# kutokana na uwepo wa laini nyingi zinazotumiwa katika matukio ya uhalifu kwa kutumia majina ya Watu wengine.

 

 

“Tunaenda Kuimarisha mifumo ya mawakala na mimi nimesema kwamba lazima makampuni ya simu yaimarishe mifumo ya Mawakala wao Sisi ikitokea uhalifu katika mtandao tutawajibisha kampuni ya Simu husika.

 

 

“Niwaombe Sana watanzania kuna hili ambao wengi wanapigwa hasa usajili wa Laini mitaani unaenda Kusajili unaambiwa weka kidole hiki oho hakijasoma weka Mara kile, kila moja pale ni Laini imesajiliwa wanaziuza kwa waharifu ikitokea tukio la uhalifu unaweza kukutwa ni wewe.

 

 

“Ndugu zangu tumetoa muda mpaka tarehe 2 Aprili 2021 haya yote nayasema yawe yametekelezwa maana wananchi wengine wanataka kuona yamefanyika leo leo tumetoa mwezi mmoja ili watu wa makampuni wakafanye marekebisho kwenye mifumo yao.

 

 

“La Tatu tulilolifanyia kazi ni wananchi walikuwa wakilalamika mabando yao kuisha kabla ya wakati hili nalo tumelitatua katika Menu ile kutakuwa na mabando yale ambayo hayana ukomo wewe ukinunua iwe ni miezi miwili au mitatu mpaka liishe.

 

 

“Kuna wale wenzangu na mimi ambao hawana uwezo, wananunua la siku au wiki tumewawekea mazingira nao mfano umenunua GB10 wiki umetumia ukaona zimebaki siku 3 ila zimebaki GB 5 unaweza kuligawa kwa Mwenzako mtandao ule ule au unaweza kununua lingine zile zikahamia kwako.

 

 

“Lakini la pili tulilolifanya ni kuhakikisha hakuna upandishaji holela tumeweka kanuni ambayo Bando likizinduliwa leo TCRA wakalipitisha hataruhusiwa kulibadilisha mpaka miezi 3 ipite ndo unaweza kuruhusiwa kubadilisha hii nayo italeta stability katika soko.

 

 

“Naingia Ndani ya wizara hii hatukuwa na bei elekezi ya mabando, hayakuwepo kama ilivyo kwenye mafuta au umeme lakini kwa utaratibu huu tumetoa bei elekezi ya Data itaanzia shilingi 2 hadi 9 makampuni ya simu hayapaswi kwenda zaidi ya hapo kwa MB Moja,” amesema Ndugulile.

 

 

Leave A Reply