The House of Favourite Newspapers

Serikali Yaanika Makubwa Iliyotekeleza, Mikakati Mipya – Video

0

KATIKA kipindi cha miaka mitano, hadi Februari 2021, serikali ya awamu ya tano imefanikiwa kutekeleza jumla ya miradi 1,845 yenye thamani ya Sh trilioni 1.916.

 

Hayo yamesemwa leo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Hassan Abbai ambapo alisema kati ya miradi hiyo, miradi 222 ni ya mijini na miradi 1,623 ni ya vijiji na imeweza kuwanufaisha wananchi 14,726,600.

 

 

“Sasa kazi inaendelea kwa sasa kuna jumla ya miradi 924 yenye thamani ya shilingi Trilioni 2.212 kwa maeneo ya mijini ni miradi 110 na kwa vijijini ni miradi 814. Miradi hiyo ikikamilika inatarajiwa kunufaisha wananchi wapatao 12,077,450,” alisema Dk Abbasi

 

Dk Hassan Abbasi amesema mapato ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa) kwa mwaka yameongezeka kutoka Sh bilioni 70.19 mwaka 2015/16 hadi Sh bilioni 137.573 mwaka 2019/20.

 

 

Dk Abbasi amesema mafanikio hayo yametokana na uamuzi mgumu uliofanywa na serikali mwaka 2017 wa kuziunganisha Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) iliyoanzishwa kwa Sheria ya DAWASA namba 20 ya mwaka 2001 na lililokuwa Shirika la Huduma ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO).

 

 

Alisema kuunganishwa kwa DAWASA na DAWASCO kumeleta mafanikio kiutendaji katika kuboresha utoaji wa huduma za majisafi na usafi wa mazingira katika Jiji la Dar es Salaam na maeneo ya Mkoa wa Pwani.

 

 

Ujenzi wa Daraja la Tanzanite (kilometa 1.03) ambalo linapita katika Bahari ya Hindi kuunganisha eneo la Agha Khan pamoja na Coco Beach, Dar es Salaam umefikia asilimia 70.6 na linatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.

 

 

“Serikali imechapa na kusambaza nakala 4,443,586 za vitabu vya Kiada, masomo yote darasa la saba katika uwiano wa 1:2 kwa wanafunzi na nakala 253,408 za Kiongozi cha Mwalimu darasa la saba katika Halmashauri zote nchini,” Dk Hassan Abbasi, Msemaji Mkuu wa Serikali.

 

 

Aidha, Dkt. Abbasi amesema Serikali itaendelea kutoa fursa na kuwaamini zaidi wanawake na watoto wa kike katika nafasi za uongozi kwenye taasisi za umma kwa kuwa siku zote wameonesha upendo, uchapakazi, uzalendo, umakini na utekelezaji uliotukuka.

 

Amesema wanawake wameendelea kuvunja rekodi ya kushika nafasi kubwa za kiuongozi hapa nchini akiwemo Makamu wa Rais, Samia Suluhu na Mhandisi Zena Ahmed ambaye kwa sasa ni mwanamke wa kwanza kuwa Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar.

 

Leave A Reply