The House of Favourite Newspapers

Serikali Yatoa Onyo Kwa Magazeti ya Mwananchi

Dkt. Hassan Abbasi.

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imetoa onyo kwa magazeti ya Mwananchi na The Citizen kwa kuyataka yajitafakari kwa kile ilichoeleza kuwa wameandika habari za “uongo wa karne”.

 

Akitoa onyo hilo, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi Hassani kupitia ukurasa wake wa Twitter, amesema kuwa magazeti hayo kwenye matoleo yake ya mtandaoni yalichapisha habari za uongo, huku wakitumia takwimu zisizo rasmi.

 

Ufafanuzi: Jana magazeti ya the Citizen na Mwananchi matoleo ya mitandaoni yalibeba habari iliyodai wahisani wametoa 6.7% tu kwenye bajeti. Habari hii ni uongo wa karne. Takwimu zilizowekwa hata kwenye viambatishi vya hotuba ya Waziri zinaonesha imetolewa 69% kufikia Jan., 2019.

Kwa makosa haya yanayojirudiarudia na yenye nia ovu (kwa kuwa hawakutaka hata ufafanuzi wa Serikali au nyaraka), Serikali inayapa nafasi ya mwisho magazeti ya Mwananchi na the Citizen kujitafakari tena kama yana sababu, nia na dhamira ya kuendelea na kazi hii.

Dkt. H.A.

Onyo hilo linakuja ikiwa ni wiki moja imepita, tangu gazeti la The Citizen kurejea mtaani, baada ya kufungiwa kwa wiki moja na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Comments are closed.