The House of Favourite Newspapers

SFC Band yawaumizia kichwa Yamoto

0

 

Stori: Mwandishi Wetu

Bendi inayokwenda kwa jina la Special Force Classic (SFC) inayoundwa na vijana machachari ambao ni Sila B, Totie, Rwegojat na Tizo chini ya uongozi wake Prince Kalawa iliyojichimbia Lushoto mkoani Tanga, inakuja kwa kasi na sasa inaumiza kichwa kuwafunika Yamoto Band.

Bendi hiyo ambayo tayari inafanya poa na ngoma zake kama vile Nimekolea na Baby la Mimi imekuwa ni gumzo kila inapofanya shoo mikoa mbalimbali na meneja wake, Prince Kalawa anasema:

“Tumejipanga kulikamata soko la muziki, tunaumiza vichwa kutoa nyimbo nzuri na video poa ili tuzifunike bendi zilizotutangulia ikiwemo Yamoto na tutafanikiwa kwani kazi inayofanywa na vijana wangu si ya kitoto.”

Leave A Reply