The House of Favourite Newspapers

SGA Yapata Tuzo Kwa Kutoa Huduma Bora

0
Mkurugenzi Mtendaji wa SGA Security, Eric Sambusa (wa pili kushoto) akionesha Tuzo ya Huduma Bora ambayo kampuni hiyo ilipokea jinini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine kutoka kushoto ni Elizabeth Muzo kutoka Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mkurugenzi wa Biashara za Kimataifa na Diplomasia ya Uchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi John Ulanga na Mkurugenzi Mkuu wa CICM Global ya Zimbabwe, Rinos Mautsa.

Kampuni ya Ulinzi ya SGA imepokea tuzo ya Huduma Bora wakati wa sherehe za utoaji wa tuzo kwa huduma bora katika ulinzi binafsi kwa mwaka 2024 jijini Dar es Salaam.

Katika tuzo hizo zilizoandaliwa na Taasisi ya Mkataba wa Usimamizi wa Wateja, kampuni kongwe ya ulinzi binafsi ya SGA nchini ilitambuliwa kwa ubora katika utoaji wa huduma bora za ulinzi binafsi nchini.

Wakati wa kupokea tuzo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ulinzi ya SGA, Bw Eric Sambu, alionyesha furaha, akisema tuzo hiyo ni ushahidi kwamba kampuni ya SGA ilikuwa ikitekeleza mkakati wake wa kutoa huduma bora. Alisema kituo cha utoaji wa huduma kwa mteja saa 24 pamoja na kutoa huduma ya dharura kinasaidia timu za kutoa huduma ya dharura zilizogawanywa sehemu mbalimbali katika majiji makuu nchini.

Mkurugenzi wa Biashara za Kimataifa na Diplomasia ya Uchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi John Ulanga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa Tuzo za Huduma Bora Jijini Dar es Salaam.

“Tumewekeza katika mifumo na vifaa kuhakikisha tunatoa huduma za hali ya juu. Tumewawezesha wafanyakazi wetu kutoa huduma kwa wateja kwa kujitoa kwani hii ni muhimu, hasa katika huduma nyeti kama ulinzi,” aliongeza.

Kampuni ya Ulinzi ya SGA ilikuwa kampuni binafsi ya kwanza kutoa huduma zake Tanzania na inaadhimisha miaka 40 mwaka huu. Ina wafanyakazi zaidi ya 5,000 Tanzania katika mtandao wake wa utoaji wa huduma. “Siri ya mafaniko yetu Tanzania ni watu wetu. Tunawekeza sana katika kuwaandaa kutoa huduma kwa wateja na kuandaa mazingira rafiki kwao na hii hutupa mafanikio makubwa. Hii tuzo ni yao wote,” Bw Sambu aliongeza.

Wakati wa utoaji wa tuzo, Mkurugenzi wa Biashara za Kimataifa na Diplomasia ya Uchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi John Ulanga aliwasihi wafanyabiashara wote kuwa na huduma kwa mteja kwani ni muhimu katika uendelezaji wa biashara zao. Aliwasihi kuwekeza katika teknolojia ili kuboresha utoaji wa huduma kwa mteja, huku akisisitiza kwamba muundo wa uchumi wa Tanzania umebadilika sana kwa kipindi cha miaka 30 iliyopita.

Kwa mujibu wa waandaaji, washindi kwa Huduma Bora Tanzania (TSEA) mwaka 2023 wanachaguliwa kupitia mchakato makini unaohusisha utafiti wa kimtandao, tathmini ya siri ya ununuzi dukani, uamuzi, na sherehe za tuzo zilizoandaliwa kwa umakini.

Ni mara ya kwanza kwa kukio kama hili hapa Tanzania, lakini limefanyika tayari katika nchi 19 Afrika na linaendelea kukua.

Leave A Reply