The House of Favourite Newspapers

SGA Yaunga Mkono Upimaji wa VVU kwa Hiari

0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya SGA Tanzania, Eric Sambu akipokea vifaa vya kupima virusi vya ukimwi kazini kutoka kwa muuguzi wa kampuni hiyo Jesca Pande punde baada ya mpango huo kuzinduliwa rasmi na Chama Cha Waajiri Kazini (ATE) kwa kushirikiana na PSI Tanzania, TACAIDS na Wizara ya Afya katika viwanja vya SGA.

 

 

 

KAMPUNI ya ulinzi ya SGA imeanzisha mpango wa upimaji wa virusi vya Ukimwi mahali pa kazi kwa wafanyakazi, hafla iliyozinduliwa katika makao makuu ya kampuni hiyo hivi karibuni.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya SGA Tanzania, Eric Sambu akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa uzinduzi wa mpango wa upimaji wa VVU kazini uliosimamiwa na wawakilishi kutoka Chama Cha Waajiri Kazini (ATE) kwa kushirikiana na PSI Tanzania, TACAIDS na Wizara ya Afya katika viwanja vya SGA Jijini Dar es Salaam.

 

 

 

Uzinduzi huo uliendeshwa na maofisa kutoka chama cha waajiri nchini ATE, PSI Tanzania, TACAIDS pamoja na maofisa kutoka wizara ya afya, ambapo uongozi wa kampuni hiyo ulipewa vifaa ambavyo wafanyakazi watapata fursa ya kujipima kwa hiari.

Baadhi ya wawakilishi kutoka Chana cha Waajiri nchini ATE, PSI Tanzania, TACAIDS pamoja na maofisa kutoka wizara ya afya wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa SGA Tanzania baada ya uzinduziwa mpango wa upimaji wa VVU kazini katika viwanja vya SGA Tanzania Jijini Dar es Salaam.

 

 

 

Uongozi wa kampuni hiyo unatarajiwa kuhifadhi vifaa hivyo ambapo inatarajiwa kuwa vitatoa mwamko kwa waajiriwa kujipima wenyewe wawapo majumbani mwao ili kujua hali zao kiafya kuhusiana na maswala ya VVU na Ukimwi kwa ujumla.

 

 

Akikabidhi vifaa hivyo, mwakilishi wa ATE katika hafla hiyo Bi Hellen Mkwizu, alisema kuwa ATE inakusudia kuwezesha waajiri kujali afya za wafanyikazi wao kwa kupima hali zao kiafya ili waweze kujitunza pale wanapobaini wako salama au wachukue zinazostahili watakapojijua wameathirika.

Alitoa rai kwa waajiri wengine kuiga mfano wa SGA utakaowawezesha wafanyikazi wao kujua hali zao na kuyalinda maisha yao.

 

 

Aliongeza, “Lengo la serikali kupitia wizara ya afya ni kufikia takwimu za 95:95:95, ambayo ni asilimia 95 ya kubaini walioambukizwa VVU, asilimia ya waliogundulika kuwa na VVU kupata matibabu na asilimia 95 ya walioathirika kutumia dawa za kurefusha maisha (ARVs)”, alisema.

 

 

Alisema ni matumaini yake kuwa mpango huo ulioanzishwa na SGA utakuwa wa manufaa makubwa kwa wafanyakazi wake, ambapo alisema ni mfano kwa waajiri wengine.

 

 

Mkurugenzi wa PSI Tanzania Bw. Ajuae Hassan, aliishukuru SGA kwa kuchukua hatua ya upimaji mahali pa kazi na kuwa mwajiri wa mfano katika mpango wa kupima maeneo ya kazi.

 

 

“Kampuni ya ulinzi ya SGA imedhibitisha ya kuwa ni kampuni ya mfano inayoongozawa si kama mwajiri mkubwa hapa nchini bali pia kwa kujali afya za wafanyakazi wake na mfano hai ni kukubali kuzindua mpango huu”, alisema.

 

 

Kampuni ya ulinzi ya SGA imeajiri zaidi ya wafanyikazi 6,000 kupitia mtandao wake ulionea nchi nzima. Kampuni hiyo kongwe ya ulinzi nchini ilianza shughuli zake hapa nchini mwaka 1984, wakati huo ikijulikana kama Group Four Security.

 

 

Mkurugenzi Mtendaji wa SGA Tanzania, Bw. Eric Sambu, aliwakaribisha washirika katika mpango huo ambayo kampuni ya SGA ilipata fursa ya kuandaa uzinduzi wake.

 

 

“Siri kubwa ya mafanikio yetu inatokana na uongozi wa kampuni kujali ustawi wa wafanyikazi wetu ikiwemo kujali afya zao wawapo kazini ikiwemo kupitia mpango huu ambao mfanyakazi atapta fursa ya kujua hali yake ya afya kwa ubinafsi wake na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa matokeo atakayopata baada ya kujipima”, alisema.

 

 

Bw. Sambu aliendelea kusema kuwa SGA inatoa kipaumbele maboresho kwa wafanyakazi na ustami wao kwa ujumla ili kuwaridhisha na hivyo kupata motisha ya kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

 

 

“Uongozi unahakikisha kuwa wafanyikazi wanapata fidia na haki zao stahiki pale inapohitajika, pia tunahakikisha wanafanya kazi katika mazingira salama kiafya, wanapewa majukumu yanayondana na taaluma zao husika na kuzikuza tena kwa Uhuru bila ubaguzi wa aina yoyote”, alisema.

 

 

Kwa upande wake Meneja wa Afya na Usalama wa SGA, Bw. Dickson Webi, alisema afya njema na usalama wa kutosha kwa wafanyakazi umeisaidia kampuni hiyo kufikia malengo yake ya mafanikio inayojiwekea, ambapo alisema kuwa hatua hizo huepelekea wafanyakazi kufanya kazi kwa moyo mmoja jambao hupunguza vitendo viovu kazini kama vile utoro, ajali, wizi na hujuma mahali pa kazi.

Leave A Reply