The House of Favourite Newspapers

Shabiki Simba akomba mil 157 za M-Bet

Meneja masoko wa M-Bet, Allen Mushi (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi Msafiri Shafii baada ya kushinda.

KAMA utani vile shabiki wa Simba, Msafiri Shafii ameibuka milionea baada ya kushinda zaidi ya milioni 157 za Kampuni ya M-Bet baada ya kushinda Perfect 12.

Shafii ameshinda Perfect 12 ya Julai 27 na kuwa miongoni mwa Watanzania ambao wamejishindia fedha kutoka Kampuni ya M-Bet kwa mwaka huu.

Meneja masoko wa M-Bet, Allen Mushi amesema: “Kama unavyojua M-Bet tumekuwa tukiendelea kutoa washindi mbalimbali wa Perfect 12 na hivi karibuni, Msafiri ndiye aliibuka mshindi baada ya kutabiri kwa usahihi timu 12.

Msafiri (kati) akishangilia wakati akikabidhiwa mfano wa hundi ya fedha alizojishindia.

“Huyu anakua mshindi wa saba wa Perfect 12 kwa mwaka huu, na bado tutaendelea kutoa washindi mbalimbali ambao watashinda. Zaidi ya bilioni 1 hadi sasa zishatoka kwa washindi hao.

“Msafiri yeye amekuwa mshindi wa Perfect 12 ya Julai 27 ambapo alitabiri timu zake kwa usahihi. Tunawasisitiza watu mbalimbali waendelee kucheza na sisi, na kitu kikubwa ni kwamba msimu mpya wa ligi ya England unakuja hivyo wana nafasi ya kucheza Perfect 12 ya M-Bet na kujishindia,” alisema Allen.

Msafiri (katikati) akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutambulishwa mshindi wa Perfect 12 ya M-Bet. 

Kwa upande wake, Msafiri alisema: “Ninawashukuru M-Bet kwa hili, mwanzoni waliponipigia kwamba nimeshinda sikuamini nikaenda kumueleza baba, lakini baadaye nimeamini na niwaambie watu waendelee kucheza na M-Bet.

“Nitakuwa balozi mzuri wa M-Bet kwetu Dodoma na pia nitaenda kuzitumia vizuri fedha hizi ambazo nimejishindia kutoka M-Bet,” alisema Msafiri aliyeshinda milioni 157,281,660.

 

Comments are closed.