The House of Favourite Newspapers

Shabiki Simba: Kwa Yanga hii, TFF watapata tabu sana msimu huu

0

 

Shabiki maarufu wa Klabu ya Simba, anayefahamika kwa jina la Mchome amesema kuwa msimu huu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi (TPBL) watakuwa na kazi ngumu kuchagua nani awe mchezaji bora.

Mchome amesema kuwa, wachezaji wengin wa Yanga wanafanya vizuri jambo ambalo litawasumbua TFF kuchagua nani wampe tuzo hiyo.

“Katika watu wana kibarua kigumu msimu huu ni bosi ya ligi na TFF, Yanga kuna watu wamewaka. Kwenye tuzo ya mchezaji bora wanaingia watu watano, wanne Yanga; Pacome Zouzoua, Aziz Ki, Khalid Aucho na Mudathir Yahya na mmoja Azam ambaye ni Feisal Salum ‘Fei Toto’.

“Lakini Feisal hauwezi moto wa mudathir yahya, moto wake umewaka vibaya mno, pale katikati haelewekei anacheza namba ngapi, sasa unamfananisha na Fei Toto?

“Mudathir ni kiungo mkabaji na mchezeshaji ni Aziz KI. Mudathir ni kama Fabrice Ngoma, muangalie Ngoma ana mabao mangapi CAF? Hana… lakini tazama Mudathir anatoka nyuma anakuja kufunga, anaonekana kwenye kila tukio.

“Mudathir akiwa hana mpira ni hatari mno kuliko akiwa na mpira, naenda sana mechi za Yanga kwa sababu napata burudani ya soka,” amesema Mchome.

 

Leave A Reply