The House of Favourite Newspapers

SHAMSA FORD, ATESWA NA KUMBUKUMBU ZA KIFO CHA ADAM KUAMBIANA!

0

KUNA nyakati tatu katika maisha ya binadamu; nyakati ya kuzaliwa, kuishi na kufa, lakini wakati huu wa mwisho unaumiza sana na siku zote husababisha machozi kwa wanaobaki. Diva anayebamba vilivyo kunako Bongo Muvi, Shamsa Ford, ameonyesha hisia za kuumisi uwepo wa muigizaji mwenziye na muongozaji wa filamu, Adam Kuambiana, ambaye alifariki miaka kadhaa iliyopita.

Picha ya Marehemu Adam Kuambiana Enzi za Uhai Wake

Shamsa alishindwa kujizuia na kuonyesha hisia za kumkumbuka marehemu Kuambiana kwa kuposti kipande cha video ya muvi waliyowahi kucheza pamoja na kukiambatanisha na maneno yanayoashiria wazi kuwa kammisi rafiki yake huyo.

HISTORIA YAKE KWA UFUPI

Marehemu Adam Philip Kuambiana alizaliwa, Juni 6, 1976 huko Ifunga mkoani, Iringa. Amepata kuonekana katika filamu mbalimbali, lakini umaarufu wake hasa ulianza mwaka wa 2007 baada ya kucheza filamu ya Fake Pastors.

Kushoto ni Marehemu Adam kuambiana Enzi za Uhai Wake, Akiwa Lokesheni

Filamu nyingine alizowahi kucheza na kumpatia umaarufu mkubwa ni pamoja na Uliyemchokoza Kaja, Danija, Mr Kadamanja, Regina, Mr Nobody na nyingine nyingi.

SABABU ZA KIFO CHAKE

Alifariki dunia Mei 17, 2014, huku ripoti ya polisi ikionesha sababu zilizopelekea kifo chake ni vidonda vya tumbo na unywaji mwingi wa pombe bila kula.

Picha za Mazishi ya Adam Kuambiana

Mungu ailaze roho ya marehemu Adam Kuambiana mahali pema peponi Amina.

NA ISRI MOHAMED/GPL

Leave A Reply