The House of Favourite Newspapers

DOGO JANJA: UWOYA KANIGOMBANISHA NA DEMU WANGU!

0

 

HIT maker wa ngoma ya Ngarenaro, Abdulaaziz Chende ‘Dogo Janja’, amefunguka kuwa skendo inayosambaa ikimhusisha yeye na Queen wa Bongo Muvi, Irene Uwoya, kuwa wanavunja amri ya sita kisirisiri, ishu hiyo imeleta mgogoro wa kukata na shoka kati yake na mpenzi wake, ambaye anadhani huenda labda ishu hiyo ina ukweli ndani yake.

Dogo Janja ambaye hata ashikiwe mtutu wa bunduki, hajawahi kukubali kuwa ni Kiben-ten wa Uwoya, alifunguka:

“Sina uhusiano wa kimapenzi na Uwoya, kwanza hii ishu imeniletea ugomvi na Mamlai wangu {mpenzi wake}, ni stori ambazo zipo nazisikia, Uwoya ni mshikaji wangu tu tunawasiliana mara chache sana, lakini mapenzi naye sina.”

 

NA ISRI MOHAMED/GPL

 

Leave A Reply