The House of Favourite Newspapers

Shamsa: Sitaki Tena Ndoa, Nilishatoka Huko

0

MMOJA wa mastaa waliofanya vizuri kupitia Bongo Muvi, ni Shamsa Ford.Mwanadada anajua kuvaa uhusika anaopewa na muongozaji wake kwenye fi lamu, kama alivyoweza kuvaa husika kwenye filamu ya Chausiku na kutokea kupendwa na kuzidi kumpa umaarufu.

 

Shamsa ambaye ni mama wa mtoto mmoja wa kiume, alisema kuwa kikubwa kwenye maisha yake ya kila siku, ni kutojipa stress.

 

ANASEMA; amechagua furaha kwenye maisha yake hata kama hana hela.Fuatilia mahojiano ya ana kwa ana na AMANI, kama yafuatayo:

AMANI: Habari Shamsa?

SHAMSA: Salama tu, niambie, una mpya gani maana mpaka umenitafuta kuna kitu.

AMANI: Hapana ni kwa ajili tu ya kuzungumza mambo ya hapa na pale na ya kipindi cha nyuma ulipokuwa mke wa Chidi.

 

SHAMSA: Maisha kwangu yanaenda vizuri sana, hakuna kilichobadilika kwangu hata kidogo, sanasana nimejifunza zaidi kujipa furaha mimi kama mimi na nimeona ninaweza kabisa.

 

AMANI: Kivipi?

 

SHAMSA: Unajua kuna wengine wanaamini kuwa furaha yako anatakiwa akupe mtu, kumbe furaha yako unatakiwa ujipe mwenyewe, kama mimi hapa naishi maisha mazuri kwa sababu nimeamua kujipa furaha mwenyewe, siendekezi Stress zisizo na lazima hata kidogo.

 

AMANI: Hujawahi kukumbuka maisha ya ndoa ulioishi hata mara moja?

 

SHAMSA: Hapana na nimesahau kila kitu, naangalia mbele siku zote kwenye maisha yangu yajayo maana nyuma yalishapita kitambo.

 

AMANI: Kwa hiyo sasa hivi uko singo?

 

SHAMSA: Hapana, nina mtu wangu, lakini si kwamba tutaoana hapana, tunapeana kampani na mawazo mbalimbali tu.

 

AMANI: Na akitaka kukuoa sasa kwa mara nyingine?

 

SHAMSA: Mimi sitaki kabisa hayo mambo ya kuolewa, nishatoka huko.

 

AMANI: Vipi biashara yako ya madera inaendeleaje?SHAMSA: Kwa kweli inaendelea vizuri sana na Mungu anasaidia kila kunapokucha.

 

AMANI: Nimeona umenunua gari lingine, ni kutoka hapohapo kwenye duka la madera pambe?

 

SHAMSA: Ndiyo na sasa hivi nimejifunza kitu kikubwa sana hakuna anayehonga, ukihongwa sana laki, sasa hiyo laki unanunua gari kweli, ndiyo maana sasa hivi kila staa anashughulika, maana maisha yashakuwa magumu.

 

AMANI: Vipi kuhusu baba mtoto wako Dick, anatoa matumizi ya mtoto kama ipasavyo?

 

SHAMSA: Nilishamsahau kabisa, kwa sababu toka mwanzo namhudumia mimi mtoto wangu, nahisi ameshajisahau kama ana mtoto alizaa sehemu.

 

AMANI: Huyu ambaye huko naye hivi sasa, huna mpango wa kuongeza naye mtoto hata mmoja?

 

SHAMSA: Bado kwanza maana isije ikawa kama huko nyuma maana raha ya mtoto awe na baba anayemjali kwa kila kitu.

 

AMANI: Vipi kuhusu bifu lako na Aunt Ezekiel, limeishia wapi?

 

SHAMSA: Sasa hivi tuko poa kabisa, tunaendelea kama kawaida. Yale ni mapito, kikubwa zaidi namuombea ajifungue salama salmini.

 

AMANI: Umekuwa mtu wa msimamo tangu miaka mitano iliyopita, ambapo ulikuwa Chadema, huku wasanii wenzako wote walikuwa Chama Tawala cha CCM,vipi kwa hivi sasa umesharudi kundini?

 

SHAMSA: Yaani mimi sasa hivi sina chama chochote niponipo tu, atakayechaguliwa Oktoba 28, ndiyo wangu.

 

AMANI: Mara nyingi umekuwa ukisemwa kwenye mitandao kuhusu mavazi yako, Kwa sababu tu unavaa nguo fupi sana, unazungumziaje hilo?

SHAMSA: Haya ndiyo mavazi yangu na siwezi kubadilika hata kidogo, waseme tu na baa

Leave A Reply