The House of Favourite Newspapers

Shangwe la Wachezaji wa Stars Baada ya Ushindi (Picha +Video)

Baada ya Mpira kuisha, kocha Emmanuel Amunike alimwagiwa maji kwa furaha na watu wa benchi la ufundi. Shiza Kichuya alikuwa akicheza ngoma kwa furaha wakati mpira ukielekea mwishoni.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alitangaza mpira wa Cape Verde na Lesotho umeisha, hivyo Manula ambaye alikuwa na mpira golini akapiga magoti na kusali kabla ya kuupiga.

Aishi Manula akiwaongoza kucheza muziki baada ya ushindi.

Kama Lesotho ingeshinda, ushindi wa Stars ungekuwa hauna maana. Ilikuwa ni shangwe kwani Dennis Onyango ambaye ni kipa bora zaidi Afrika, alitunguliwa mabao matatu.

Stars imepata nafasi hiyo baada ya kuichapa Uganda bao 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mbele ya wakubwa wengi wa nchi wakiongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Kassim Majaliwa aliyekuwa mgeni rasmi wa mechi hiyo, na mawaziri kibao akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe.

PICHA NA MUSA MATEJA, GPL

Comments are closed.