The House of Favourite Newspapers

Sharobaro Yamkuta Mazito Muhimbili!

SHAROBARO mmoja ambaye jina lake halikujulikana mara moja wikiendi iliyopita alikutwa na mazito ndani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar baada ya kushushiwa kipigo cha aina yake kisa kikidaiwa ni kufanya tukio la wizi.

 

Tukio hilo lilijiri nje ya jengo la mochwari maeneo ambayo watu husubiri ili waingie kushughulikia maiti za ndugu zao ambapo kijana huyo aliyekuwa amevalia nadhifu alidaiwa kumuibia dada wa watu simu yake hivyo kujikuta akichezea kipigo.

 

Akizungumza na gazeti hili, shuhuda aliyejitambulisha kwa jina moja la Hamisi Kudu alisema kijana huyo alikuwa amekaa sambamba na binti ambaye jina lake halikujulikana ambapo alimchomolea simu pamoja na pesa kwenye pochi yake.

 

Aliendelea kudai kuwa, binti huyo alishituka baada ya kugundua kuwa, yule kijana aliyekuwa amekaa naye alikuwa amemfanyia kitu mbaya kwa kumuibia simu pamoja na pesa (vilikuwa kwenye kipochi).

 

“Yule sharo alipobanwa akatoa pesa lakini simu hakutoa ndiyo maana watu wakampa kipigo mpaka kuloa damu chapachapa, kama siyo kuokolewa na walinzi wa hapa hospitali na kupelekwa kwenye chumba chao kwa mahojiano, angeweza kufa hapahapa,” alidai shuhuda huyo.

 

Wakati sharobaro huyo akishushiwa kipigo alisikika akidai kwamba alifika mahali hapo kwa ajili ya kusubiri muda wa kuingia wodini kuwasalimia ndugu zake ambao ni wagonjwa.

 

Jitihada za kuzungumza na kijana huyo hazikuzaa matunda baada ya walinzi wa eneo hilo kumficha kumuepusha na kifo.

Gladness Mallya, Risasi Mchanganyiko.

Comments are closed.