The House of Favourite Newspapers

Sheikh Mkuu Aomba Waumini Dini Zote Kuchangia Ujenzi wa Msikiti

0
Imam wa msikiti huo (kulia) akisoma risala kwa mgeni rasmi Katibu Tawala Wilaya ya Nachingwea Lindi, Omary Mwanga (kushoto).

SHEIKH Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi, Abdul Mpakate amewaomba waumini wa dini ya kiislamu na raia wote wenye mapenzi mema na dini hiyo na dini nyingine kuchangia ujenzi wa msikiti wa Masjid Annur uliopo Kijiji cha Naipanga mkoani humo ambao unahitaji kumaliziwa ulipoishia kwa nguvu ya wananchi wa kijiji hicho.

Akizungumza kwenye hamasa ya ujenzi wa msikiti huo hivi karibuni, Sheikh Mpakate aliwaomba raia wote wenye mapenzi mema kuchangia kumalizia ujenzi wa nyumba hiyo ya kumuabudia Mwenyezi Mungu.

Diwani wa kata hiyo, Geofrey Kambona akizungumza kwenye hafla hiyo.

Sheikh huyo alitoa rai kuwa yeyote mwenye mapenzi mema na ujenzi huo afike msikitini hapo na kuonana na kamati ya ujenzi huo na kwa waliombali watume michango yao kupitia akaunti ya Benki ya NMB yenye namba 70410005647 Jina la akaunti Masjid Annur.

Ameendelea kusema kuwa kwa waotumia mihamala ya simu wanaweza kutuma pesa za ujenzi huo kupitia namba 0714 004134 litatokea jina la Twaha Munyuku ambaye ni Katibu wa Kamati ya ujenzi huo. Alisema Sheikh huyo.

Katibu Tawala, Wilaya na Nachingwea mkoa wa Lindi, Omary Mwanga akizungumza kwenye hafla hiyo.

Katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Nachingwea, Omary Mwanga ambaye naye alitumia nafasi hiyo kuwahamsisha wananchi mbalimbali kuunga mkono harakati za ujenzi wa msikiti huo.

Sehemu ya waumini wakifuatilia yaliyokuwa yakiendelea kwenye hafla hiyo.

Baada ya kutoa hamasa hiyo alichangia mifuko ishirini ya sementi kwa niaba ya wilaya hiyo na kuahidi kuendelea kuwahamsisha wengine kwenye wilaya yake na kwingineko kuchangia ujenzi huo ambao ulijengwa kwa nguvu ya wanakijiji hao na kuishia hapo.

Waliohudhuria hafla hiyo wakimzunguusha mgeni kumuonesha ujenzi wa msikiti huo ulipofikia.

“Nawasihi wananchi wote popote walipo kuchangia ujenzi wa msikiti huu mahali ambapo ni pakumuabudia Mwenyezi Mungu na kujifunzia yaliyo mema ili kesho tuweze kufikia mahali pema peponi”. Alisema Katibu Tawala huyo.

HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL     

Leave A Reply