The House of Favourite Newspapers

Sheikh Walid Na Padri Mtweve Kuongoza Dua Jumamosi Hii Leaders Club

0

Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Walid Alhad Omar na Padri Nestory Mtweve wataongoza dua ya kuwaombea na kuwarehemu ndugu jamaa na marafiki wa Club za Michezo za Tazara, Singasinga, Sigara , Checkpoint, Mango Garden na Maasai Club ambao wametangulia mbele ya haki katika Viwanja via Leaders Club Jijini Dar es Salaam kesho Jumamosi kuanzia saa tano asubuhi.

Kwa Mujibu wa Richie Dillon, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya shughuli kwa pamoja na kamati nzima wakiwemo:
– Jeff Nasser – Katibu
– Amir Rashid – Mjumbe
– Hamis Kindoroko – Mjumbe
– Martin Ngadada – Mjumbe
– Muhidini Issa Michuzi – Mjumbe
– Maxi Rutihinda – Mjumbe
– Nestor Mapunda – Mjumbe
– Joe Holela – Mjumbe ambayo iliasisiwa mwaka 2011 na aliyekuwa Mkuu wa Itifaki Marehemu Balozi Cisco Mtiro, maandalizi na Mipango yote yamekamilika kwa asilimia 99, ikiwa ni pamoja na ma-tent ya kutosha iwapo kutakuwa na mvua, na kwamba wanategemea safari hii wadau watajitokeza kwa wingi zaidi.

Dillon amesema baada ya viongozi hao wa dini kuongoza Sala na Dua wahudhuriaji watapatiwa chakula cha mchana na vinywaji baridi huku wakisindikizwa na burudani ya tarabibu toka kwa Dj Bonny Love.

Hayati Cisco, akishirikiana na wakuu wa vilabu hivyo vya Michezo vya Tazara, Singasinga, Sigara, Checkpoint, Mango Garden na Masai Club alibuni hafla hii ili kuwakumbuka wanachama waanzilishi wa Tamasha la kila Jumapili la Sunday Soccer Bonanza waliotangulia mbele ya haki.

Tamasha hilo, lililozinduliwa na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho kikwete (Wakati huo akiwa Waziri wa Mambo ya Nje) mwaka 1997 ni la kila mwaka na hujumuisha wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na wanamichezo veterani na wa sasa, wanamuziki wa kada zote ikiwa ni pamoja na muziki wa Dansi, bongofleva, disko na taarabu.

Wengine ni wasanii wa Bongo movie, utamaduni na wachoraji pamoja na wanasiasa, wafanyabiashara na wadau wa kila aina.

“Hili ni tamasha la watu wote kwani wanafamilia, ndugu, jamaa na majirani wa marehemu wapendwa wetu hao wamealikwa.

“Pia tuna mikakati ya kuifanya hafla hii liwe kubwa zaida na ya Kitaifa huko siku za mbele” , alisema Dillon.

Leave A Reply