The House of Favourite Newspapers

Makatibu Wakuu Wafanya Ziara Handeni Wanapohamia Wakazi wa Ngorongoro

0

 

Makatibu Wakuu ziarani Msomera Handeni leo ambako uwekezaji na uwezeshaji wa kihistoria unaendelea chini ya Serikali ya Awamu ya Sita mahali wanapohamia wakazi wa Ngorongoro.

1. Kila kaya inapewa nyumba ya vyumba vitatu;
2. Fidia ya maendelezo wanakotoka;
3. Fedha ya usumbufu;
4. Eneo la eka 2.5 la kiwanja chenye hati;
5. Shamba eka 5 na hati;
6. Gharama za usafiri wa familia nzima na mifugo kutoka Ngorongoro hadi hapa
7. Chakula cha miezi 18 ya mwanzo tangu kuhamia.

Na bado, Serikali inajenga na kuhakikisha huduma hizi eneo jipya ambazo kule Ngorongoro ama kisheria; kwa sababu za sheria za ndani au kimataifa za uhifadhi ilikuwa hawapati au haziruhusiwi kuwekwa sasa Msomera watapata pia:

1. Barabara nzuri za mitaa kwa sasa zaidi ya km 140 tayari na zitafika km 800
2. Maji zaidi ya visiwa 8 vishachimbwa
3. Umeme unaendelea kusambazwa
4. Shule ya msingi ishajengwa na nyingine inakuja
5. Shule za sekondari na maabara ya kisasa ya kompyuta inajengwa
6. Huduma za afya kituo tayari na kinakuja kingine
7. Vituo vya polisi kimoja tayari cha daraja B kinakuja cha pili
8. Mnada wa mifugo ushajengwa unakamilika


9. Mashamba ya malisho yashapimwa na shamba darasa limeanza
10. Mabwawa na maeneo ya kunywesha mifugo mawili yanajengwa moja limeshajaa maji bwerere na vituo kafhaa vya kunyweshea vishaanza kazi
11. Vituo vya kuuzia maziwa vinajengwa
12. Huduma za ustawi wa jamii
14 Kunajengwa kituo maalum kuhudumia watoto waliofanyiwa ukatili
15. Kunajengwa kituo cha huduma za pamoja (One Stop Center)
16. Maghala ya kuhifadhia malisho na raslimali za mifugo
17. Minara ya mawasiliano imewekwa
18. Kanda maalum mbalimbali zimetengwa ikiwemo korido za wanyamapori, malisho, biashara mbalimbali, michezo n.k.
19. Takribani viwanja 5,648 vimeshapimwa katika maeneo ya Msomera (Handeni), Saunyi (Kilindi) na Kitwai (Simanjiro).

Leave A Reply