The House of Favourite Newspapers

Sheria Mpya Kukamata Walevi Wanaotembea Hadharani

 

POLISI nchini Uganda inapania kuzindua mpango wa kuwakamata watembea kwa miguu watakaopatikana wakiwa walevi.

 

Akitetea mpango huo mpya,  kamanda wa trafiki katika jiji la Kampala, Lawrence Niwabiine, amesema kikosi cha polisi hakitaruhusu watu “wahatarishe”maisha yao.

 

Tayari vyombo vya habari nchini Uganda vimezua gumzo mitandaoni baada ya kuangazia mpango huo tata katika mitandao ya kijamii.

 

Watu wamekuwa wakihoji jinsi sheria hiyo itakavyotekelezwa hasa ikizingatiwa kuwa baadhi ya watu wanaokamatwa kila uchao wakiendesha magari wakiwa walevi huishia kuachiwa katika mazingira ya kutatanisha.

 

Hata hivyo,  kuna mamia ya watu waliopatikana na hatia ya kuendesha magari wakiwa walevi wakashindwa kulipa faini.

 

Gazeti la New Vision limeendeleza gumzo hilo katika mtandao wa kijamii wa Twitter kwa kuelezea sheria hiyo inayopendekeza kuwa mtu akipatikana na hatia atapigwa faini ya hadi Dola 10,000 na pia kuwauliza wasomaji wake kutoa maoni kuhusiana na pendekezo hilo.

 

Wengine wanasema hatua hiyo huenda ikawa na athari kwa uchumi wa nchi. Wanaharakati wanapendekeza mifumo ya kisheria na kijamii iwekwe sawa kabla ya kuanza kutekeleza sheria hiyo.

 

”Kabla ya kuanza mpango huo, magereza yatahitaji kupanuliwa haraka iwezekanavyo kwa sababu watu wengi walevi wanaotembea baada ya kunywa, hawana uwezo wa kulipa faini,  la sivyo mahakimu watakuwa na kibarua kigumu katika kutoa hukumu dhidi ya watu hao wakati sheria inasema kila mmoja achukukliwe hatua,” alisema mmoja wao.

 

Pili anasema wafanyabiashara wa pombe watalazimika kuhamisha biashara zao katika maeneo ya makazi ili kupunguza hofu ya wateja wao kukamatwa.

 

”Hata polisi akipiga kambi karibu na hapo akisubiri kukukamata hataweza kufanya hivyo maana  unaweza kuamua kumpigia simu mmoja wa jamaa zako nyumbani kukuletea mtu ulale ndani ya baa karibu na kwako,” ,aliongeze.

 

Pia anasema kumbi za burudani zitapoteza umuhimu kwa sababu kile ninachowavutia wateja ni pombe.  Pia wafanyabiashara wa teksi wamepokea vyema pendekezo hilo kwa sababu walevi watalazimika kutumia huduma zao za usafiri kwa kuhofia kukamatwa.

 

Baadhi ya wakazi wamewaonya wenzao wanaopenda kunywa pombe kuwa makini hata wanapotumia usafiri wa umma kwa sababu polisi huenda wakawasubiri katika stendi ya mwisho wa gari linapokwenda.

Comments are closed.