The House of Favourite Newspapers

Magufuli Amwaga Mil. 2, Atoa Siku 10 Umeme Ufungwe! – Video

RAIS John Magufuli ametoa Tsh milioni 2, kwa ajili ya kununua kinukuzi (photocopy machine) na kuvuta umeme katika Shule ya Msingi Ileje, iliyopo Rungwe mkoani Mbeya huku akitoa muda wa siku kumi kukamilika kwa zoezi hilo.

 

Magufuli ametoa pesa hizo leo Aprili 29, wakati akizindua kiwanda cha kusindika maparachichi kilichopo Wilaya ya Rungwe mkoani  Mbeya ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya siku nane mkoani humo.

 

Akizindua kiwanda hicho  alipongeza mkurugenzi wa kiwanda hiki kwa kuitikia wito wa serikali kwa kujenga Tanzania  ya viwanda ambapo aliongeza kwamba ujenzi wa uwanja wa ndege wa Songwe ni mkakati wa kusafirisha haraka mazao kwenda nchi za nje.

 

Pia alipongeza juhudi za kiwanda hicho kinachoshirikisha wakulima wapatao 20,000 wanaojishughulisha na zao la parachichi ambao hukiuzia, jambo ambalo limewanufaisha katika juhudi zao za kilimo.

 

“Nimuombe mnunuzi wa kiwanda hiki cha kusindika parachichi aanze kutoa bei nzuri kwa wakulima,” alisisitiza Magufuli.

 

NEEMA! JPM Azindua Kiwanda Cha MAPARACHICHI

Comments are closed.