The House of Favourite Newspapers

Shetta ala za chembe, kisa ‘mdendeko’ na waifu wake

0

shetta

Shetta

Stori: Hamida Hassan
Hivi karibuni msanii wa muziki, Shetta alitupia picha mtandaoni ikimuonesha akidendeka na mkewe, Mama Kaila, hali iliyomfanya ale za chembe.

Wengi walioiona picha hiyo ambayo haiko kimaadili, walimponda na kusema anamdhalilisha mama watoto wake.
Mmoja wa mashabiki wake aliyejitambulisha kwa jina la Shebby Boy kwenye Mtandao wa Instagram alisema; “Huo ni utoto, Shetta acha kumdhalilisha mkeo.”

Mwingine akadakia: “Huwezi kutafuta kiki kwa njia hii, fanya muziki mtamu, watu watakuelewa, haya mambo waachie andagraundi broo. Kwanza wewe ni Muislam, imani yako na mambo hayo ni vitu viwili tofauti.”

Leave A Reply