The House of Favourite Newspapers

Sheva Arejea Rasmi Msimbazi

0
Miraji Athumani ‘Sheva’.

HABARI njema kwa mashabiki wa Simba ni kuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Miraji Athumani ‘Sheva’ ameweka wazi kuwa amepona na tayari ameshaanza mazoezi ili kujiweka fiti kurejea uwanjani.

 

Sheva alikuwa nje kwa muda wa miezi minne akiuguza majeraha ya mguu, ambayo aliyapata wakati akiwa anatimiza majukumu ya timu ya taifa katika mashindano ya Chalenji yaliyofanyika Uganda mwishoni mwa mwaka jana.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Miraji alisema kuwa, kwa sasa anaendelea vizuri mara baada ya kupata nafuu kubwa kama siyo kupona kabisa.

 

“Namshukuru Mwenyezi Mungu nimepona kabisa na najisikia kuwa na afya njema na tayari nimeshaanza mazoezi mepesi, nilikuwa na wakati mgumu kipindi chote nilichokuwa sichezi kwani nilitamani nami niingie uwanjani lakini ndiyo hivyo isingewezekana kutokana na majeraha.

 

“Ninaendelea kufanya mazoezi binafsi kabla ya kuanza na timu kwa pamoja, nafanya hivyo ili nikirejea kikosini niweze kuendeleza pale nilipoishia na kuweza kuwapa raha mashabiki wetu ambao walinimisi,” alisema Sheva.

STORI: Issa Liponda na Marco Mzumbe

 

Leave A Reply