The House of Favourite Newspapers

Sheva: Nimerudi Kwenye Ubora Wangu

0

MIRAJI Athuman ‘Sheva’ ambaye anashikilia rekodi ya kuwa ‘super sub’ wa Simba msimu huu akiwa ameshikilia mabao ya Meddie Kagere amesema kuwa yupo fiti.Sheva kabla ya kuumia misuli ya nyuma ya enka mwaka jana alipokuwa na timu ya Taifa ya Tanzania alionyesha maajabu kwenye ligi, akifunga mabao sita huku pasi yake moja na penalti mbili alizosababisha mbele ya Mbeya City na Kagera Sugar zikifungwa na Kagere mwenye mabao 19.

 

Maajabu yote haya Sheva aliyafanya ndani ya dakika 508 alizocheza akiwa amehusika moja kwa moja kwenye mabao tisa ya Simba kati ya 63, akiwa na wastani wa kuwa na hatari langoni kila baada ya dakika 56.

Sheva ameliambia Championi Jumatano, kuwa anamshukuru Mungu ametenda maajabu kwani ameanza kurejea kwenye ubora wake.

 

“Ukweli napenda kumshukuru Mungu kwa kuwa nimeshaanza kurudi kwenye ubora wangu, naamini ligi ikianza nitakuwa moto,” alisema Sheva.Mechi alizocheza ni tisa kati ya 28 ambazo ilikuwa namna hii:-JKT Tanzania (30), Mtibwa Sugar (27) Kagera Sugar (29), Biashara United (83), Azam FC (33), Singida United (81), Mwadui (45), Mbeya City (90), Ruvu Shooting (90).

Stori: Lunyamadzo Mlyuka, Dar es Salaam

MOLINGA Amejibu KUONDOKA YANGA – “Tusubiri LIGI Irudi, MPIRA sio KUONGEA ONGEA”

Leave A Reply