The House of Favourite Newspapers

Shigongo Aendelea Kung’ara Buchosa

0

HARAKATI za mgombea ubunge Jimbo la Buchosa kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eric Shigongo, zimeendelea kung’ara ambapo Oktoba 16, mwaka huu, alifanya kampeni zake kwenye vijiji vya Bulolelo, Luharanyonga na Isagenhe.

Sehemu zote alizopita mgombea huyo hadi sasa ikiwemo Kisiwa cha Kome ilipo ngome ya mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Charles Tizeba, ameonekana kuungwa mkono kwa asilimia 100.

Mapema jana Jumamosi, Shigongo ambaye ni mdau mkubwa wa michezo akishiriki mara kadhaa kufadhili michuano mbalimbali, alizulu Kisiwa cha Maisome na kuchakaza kata zote na kuacha gumzo kubwa kwa wananchi ambao wanatarajia kumpigia kura Oktoba 28, mwaka huu katika Uchaguzi Mkuu wa Tanzania.

 

Leo Jumapili ni zamu ya kufanya kampeni kwenye Kata ya Bupandwamhela ambapo ndipo yalipo makazi ya mgombea huyo.

Leave A Reply