The House of Favourite Newspapers

Tamasha la Jiachie na ‘Kili’ Lilivyokuwa Full Mzuka Ndani ya Escape One

0
Lavalava akimchizisha shabiki.

MASHABIKI wa burudani usiku wa kuamkia leo walikuwa ‘full vibe’ ndani ya Ufukwe wa Escape One uliopo Mikocheni jijini Dar ambapo kulikuwa na tamasha la Jiachie na bia ya Kilimanjaro.

Whozu naye akiwachizisha jamaa.

Tamasha hilo ambalo limedhaminiwa na Kampuni ya Tanzania Breweries kupitia bia yake ya Kilimanjaro mashabiki waliofurika kiwanja hicho hawakuwa na kinywaji kingine zaidi ya hicho.

jamaa wakijiachia.

Yaani ilikuwa kila unapogeuka ni mambo ya kujiachia na bia hiyo tu.

Tamasha hilo lilipambwa na burudani kutoka kwa mastaa wa bongo fleva ambapo miongoni mwa waliopanda jukwaani ni pamoja na Billnass, Juma Nature, Mheshimiwa Temba, G Nako, Lavalava na wengineo kibao.

Mambo ilikuwa ni kuserebuka na kunywa mwanzo mwisho.

Sambamba na wakali hao kutoa burudani ya live kuna kipindi, DJ Jozee naye alikuwa akipata muda wa kuwapagawisha mashabiki waliofurika ufukweni hapo.

Washkaji wakifuatilia shoo kidizaini.

Yaani mambo yalikuwa ni full mzuka watu si kupagawa huko.

HABARI/PICHA:RICHARD BUKOS /GPL  

Leave A Reply