The House of Favourite Newspapers

Shigongo Amaliza Kero ya Tozo Bandari ya Lushamba Kanyala

0

Buchosa: Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo hatimaye amemaliza kero ya tozo iliyokuwa ikilalamikiwa na wananchi wanaotuma bandari ya Lushamba Kanyala.

Kupitia vikao vya hadhara vya kusikiliza kero za wananchi, Shigongo alikutana na kero hiyo alipokuwa Kijiji cha Kanyala ambapo wananchi walilalamika kuwa tozo inayotolewa na Mamlaka ya Bandari kwenye Bandari ya Lushamba Kanyala ya sh600 kuingia na sh600 kutoka kuwa ni kubwa hivyo Serikali inatakiwa kuliangalia upya.

Baada ya Shigongo kulifuatia suala hilo na Serikali kulifanyia kazi, hatimaye kilio hicho kimesikizwa na Serikali tozo hiyo imepunguzwa kutoka sh600 hadi kufikia 400.

Mbunge wa Jimbo la Buchosa Eric Shigongo.

Meneja wa Mamlaka ya Bandari Kanda ya Ziwa, Vecent Stephano amesema Serikali imesikia kilio cha wananchi na hatimaye tozo hiyo imepunguzwa.

Awali, kila mwananchi alikuwa anatozwa sh600 na sh600 anapotoka ambapo ambalo lilikuwa likilalamikiwa na wengi kuwa mzigo kwao.

Stephano amesema, Serikali baada ya kusikia kilio cha wananchi juu ugumu wa maisha na kushindwa kulipa tozo wanapotumia bandari hiyo, tozo hiyo imepunguzwa hadi sh400 kuingia na kutoka sh400.

“Suala la kupunguza tozo halikuwa dogo, Shigongo amepambana kwa kuiomba Serikali kusikia kilio cha wananchi hatimaye tozo hiyo imepungua kwenye maziwa yote yaliyoko hapa nchini,” amesema Stephano.

Wananchi wa Jimbo la Buchosa wameishukuru Serikali kwa kusikia kilio chao na hatimaye kero ya tozo kwenye Bandari ya Lushamba Kanyala kutatuliwa.

Mwandishi Wetu.

Leave A Reply