The House of Favourite Newspapers

Shigongo: Hakuna Aliyezaliwa Kuwa Maskini, Kila Mtu Anaweza Kufanikiwa (VIDEO)

0
Eric Shigongo (wa pili kushoto) akisalimia na walimu wa Shule ya Sekondari Tambaza.

MKURUGENZI wa Kampuni ya Global Publishers, Mwalimu na Mhamasishaji maarufu Afrika Mashariki na Kati, Eric Shigongo leo Alhamisi, Agosti 10, 2017 alipata fursa ya kuwatembelea wanafunzi wa Shule ya Sekondari Tambaza iliyopo jijini Dar es Salaam na kuwapa nasaha kuhusu masomo na namna ya kupambana ili waweze kufanikiwa katika maisha yao ya baadaye.

 

Wanafunzi wa Tambaza wakifuatilia mafundisho hayo.

Akizungumza wakati akitoa nasaha hiyo, Shigongo amewaambia kuwa wanatakiwa kusoma kwa bidii na kuhakikisha wanapambana ili waweze kufanikiwa zaidi kuliko wazazi wao.

Shigongo akiwaasa wanafunzi hao.

“Hakuna mtu aliyezaliwa kuwa maskini, kutokana na malengo yako, jambo la msingi ni kujiamini, kuwa na juhudi kila mtu ana uwezo wa kupambana na kufikia mafanikio mazuri.

 

Shigongo akiwapa akitoa nasaha kwa wanafunzi hao.

“Usijione kwamba hauna maana, kila mtu ana umhimu wake hapa duniani, unaweza kuwa Rais, waziri, mwanasayansi ama kiongozi mkubwa duniani, inawezekana.” alisema Shigongo.

Msanii wa Bongo Fleva, H-Mbizo akitumbuiza.

 

Msanii Harmorapa akitumbuiza.

 

Msanii maarufu wa kupiga saxophone, Moses akiweka mitambo sawa.

 

Shigongo akifafanua jambo.

 

MSIKIE SHIGONGO AKIZUNGUMZA

Leave A Reply