The House of Favourite Newspapers

Shigongo Kunogesha College Box Concert

KAMPUNI ya Global Publishers, kesho Jumamosi inatarajiwa kufanya tamasha la aina yake katika Shule ya Sekondari ya Alpha iliyopo jijini.

 

Tamasha hilo lililopewa jina la High School and College Box Concert linafanyika kwa mara ya kwanza huku dhumuni kubwa likiwa ni kuwapa elimu wanafunzi ambao wanajiandaa kumaliza elimu ya sekondari na kwenda vyuo mbalimbali.

Mbali na hilo, pia kutangaza bidhaa zinazozalishwa na Global Publishers yakiwemo magazeti, Global TV Online, +255 Global Radio na Global App.

Pacific Ibrahim ambaye ni mmoja wa waandaaji wa tamasha hilo, amesema: “Tumeona kuja na hiki kitu ili kuzifanya bidhaa zetu kufika mbali zaidi na tumelenga katika shule mbalimbali na vyuoni kwa sababu huko kuna vijana wengi wamekuwa wafuatiliaji wakubwa wa mitandao ya kijamii.

 

“Kuna mambo mengi yatafanyika ikiwemo michezo mbalimbali ambayo hii itahusisha wanafunzi wenyewe watakaoshindana, pia kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.

 

“Kwa watakaofanya vizuri katika mashindano hayo, tutawapa zawadi mbalimbali kutokana na kuthamini vipaji vyao. “Pia kutakuwa na nafasi kwa wazungumzaji mashuhuri hapa nchini wakiongozwa na Eric Shigongo ambao watazungumza na wanafunzi katika masuala mbalimbali ikiwemo kutatua changamoto zao za kimaisha.

 

“Siku hiyo tutaitumia vizuri sana kwa ajili ya kuizindua Global App ambayo kuna sehemu itakuwa maalum inayowahusu wanafunzi. Humo ndani tutaweka matukio na mambo mbalimbali yanayowahusu wao peke yao. Itaitwa College Box.”

Comments are closed.