The House of Favourite Newspapers

Shilole Ataka Kuchoma Gauni, Kisa… Bofya Hapa

Mwanamuziki wa wa miondoko ya Mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amesema gauni alilovaa kwenye uzinduzi wa kumtambulisha mwanamuziki Maromboso ‘Mbosso’ uliofanyika katika Ukumbi wa Hyatt hivi karibuni, limemtia aibu kiasi cha kutaka kulichoma moto.

 

Akizungumza na Star Mix, Shilole alisema kuwa, aliagiza gauni lile mtandaoni lakini hakujua kuwa lingemtia aibu vile kwa maana lilimkosesha kabisa raha kwenye sherehe hiyo na kujutia hela ambayo aliitoa.

 

“Jamani katika kitu ambacho kimenitia aibu kwenye gauni nililovaa siku ile sitosahau yaani mpaka sasa nataka nilichome moto kabisa nisiwe naliona,” alisema Shilole.

Comments are closed.