The House of Favourite Newspapers

SHILOLE MJAMZITO?

STAA anayefanya vizuri kwenye miondoko ya mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefungukia madai ya yeye kuwa ni mjamzito na kusema kuwa hayo ni maneno ya watu, lakini yeye yupo fiti.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Shilole alisema kuwa, amenenepa kwa ajili ya raha anazopewa na mumewe Uchebe na kuridhika na maisha yake, lakini siyo kwamba ana ujauzito.

“Watu wengi wanasema hivyo, lakini mimi sina ujauzito, bali nimenenepa tu kwa raha anazonipa mume wangu,” alisema Shilole na kudai kwamba, wanaosema hivyo siyo watu wabaya kwani wanamtakia heri na mambo mazuri.

Stori: Imelda Mtema, Dar

Comments are closed.