The House of Favourite Newspapers

Shinda Nyumba Awamu ya Pili… Kesho CCM Mwinjuma

    

DROO ya pili ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili itafanyika kesho Ijumaa katika Viwanja vya CCM Mwinjuma, Mwananyamala Kinondoni jijini Dar es Salaam. Ofisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda, alisema jana kuwa mipango yote kwa ajili ya shughuli hiyo ya pili imekamilika na kilichobakia ni kusubiri siku ifike shughuli iishe.

 

“Kitu kikubwa kilichokuwa kinatupeleka mbio ni suala la wapi tutafanyia shughuli hii, lakini sasa naweza kuthibitisha kuwa tukio hili litafanyika kesho kuanzia saa nane alasiri na tunawakaribisha wasomaji wote wa Jiji la Dar es Salaam, hasa wa mitaa ya jirani,” alisema Mkanda.

Wakati ikithibitika juu ya sehemu ya kufanyia droo hiyo inayosubiriwa kwa hamu, wasomaji wa magazeti ya Global Publishers ambayo ni Risasi, Amani, Uwazi, Ijumaa, Championi na Ijumaa Wikienda , waliendelea kujigamba kuwa huu ni wakati wao wa kujinyakulia zawadi.

“Najua ni bahati nasibu, lakini kujitabiria ushindi siyo jambo baya, maana ukisubiri mtu akutabirie mazuri utakaa sana, sasa naendelea kununua magazeti na kuhifadhi kuponi, kila ninapopata nafasi ninazipeleka mwenyewe ofisini Global, sitakaa mbali siku hiyo ili kushuhudia,” alisema Dedeki Jopi wa Bunju jijini Dar es Salaam.

Tarik Mbashau kutoka Tanga, naye alisema japokuwa atakuwa mbali siku ya kuchezwa kwa droo hiyo, ana uhakika wa kushindwa kwani uzoefu unaonyesha wanaoshinda zawadi siyo wote huwa wa Dar es Salaam, kwani katika droo iliyopita, mshindi wa pikipiki alikuwa ni mwenyeji wa Muheza, mkoani Tanga.

“Ingawa kuwepo mwenyewe eneo la tukio ni jambo zuri, lakini sisi tunawaamini sana Global, kama ni kuponi yako ndiyo imeshinda, zawadi zako utapata tu, hivyo tunaisubiri hiyo siku kwa hamu na sisi tutakuwa tunaomba dua tu tuibuke washindi,” alisema msomaji huyo.

Droo ndogo ya kwanza ilifanyika Februari 8, mwaka huu katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakhem ambako washindi watano walijishindia zawadi za pikipiki, televisheni, simu za kisasa, vyombo vya jikoni na vitu vingine vingi.

 

Washindi hao ni Andrew Mtunguja wa Muheza mkoani Tanga, Ambrosi Ligonja wa Mang’ula Morogoro, Evans Stanley wa Kunduchi, Said Mohamed na Gasto Peter wote wa Kimara jijini Dar es Salaam.

Bahati nasibu hiyo kubwa kabisa kuwahi kuchezwa na kampuni ya magazeti nchini, inadhaminiwa na Kilimanjaro Institute of Technology and Management iliyopo Mwenge kwa Mama Ngoma na Afrikasana na British School ambayo ipo karibu na Kituo cha Daladala cha ITV, karibu na Kanisa la Lutheran.

 

Comments are closed.