The House of Favourite Newspapers

Shinda Nyumba Droo Ndogo: Mshindi wa Pikipiki Akabidhiwa

0

Nyumba (8)Mshindi wa Pikipiki aina ya Skymark, Evans William akiwa na zawadi yake mara baada ya kukabidhiwa.Nyumba (1)Mwandishi wa Gazeti la Championi, Wilbert Moland akimkabidhi zawadi ya bed sheet, Marian Mwakale.Nyumba (2)Mshindi wa simu ya kisasa (smartphone), Richard Mauga (kushoto) akikabidhiwa zawadi na Wilbert Moland.

Nyumba (3)Mwandishi wa Gazeti la Championi, Wilbert Moland akimkabidhi funguo mshindi wa pikipiki aina ya Skymark, Evans William.

Nyumba (4)

Afisa Masoko Msaidizi wa Global Publishers, David Mwaipaja akifanyiwa mahojiano mara baada ya washindi kukabidhiwa zawadi zao.

Nyumba (5)

Mwandishi wa Gazeti la Champion, Wilbert Moland akimkabidhi zawadi ya seti ya vyombo vya nyumbani, Eginita Nsemwa kwa niaba ya mshindi, Akani Nsemwa.

Nyumba (6)Mshindi wa simu ya kisasa (smartphone), Richard C. Mauga akifanyiwa mahojiano na MC Chaku.

Nyumba (7)Mshindi wa bed sheet, Marian N. Mwakale akifanyiwa mahojiano na MC Chaku mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake.

Nyumba (9)Washindi wa Droo Ndogo ya Mwisho wakiwa na zawadi zao katika picha ya pamoja.

KAMPUNI ya Global Publishers ambao ni wachapishaji wa Magazeti ya Risasi, Championi, Ijumaa, Amani, Uwazi na Ijumaa Wikienda leo wamekabidhi zawadi ya Pikipiki aina ya Skymark kwa mshindi wa Droo Ndogo ya Mwisho ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba, Evans William.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo katika Ofisi za Global Publishers zilizopo Bamaga-Mwenge jijini Dar, Evans ambaye ni fundi magari alisema kuwa ni mfuatiliaji mzuri wa Magazeti Pendwa na Championi na alijitahidi kucheza mara kwa mara kila alipokuwa akinunua gazeti.

“Sijui hata nielezeaje, kifupi nilichanganyikiwa kwa muda, sikuamini kabisa kama nimeshinda pikipiki,” alisema Evans.

Naye Ofisa Masoko Msaidizi wa Global Publishers, David Mwaipaja alisema kuwa zimesalia wiki chache hivyo kuwaomba wasomaji wa Magazeti ya Amani, Uwazi, Championi, Risasi, Ijumaa na Ijumaa Wikienda kusoma kwa wingi na kujikatia kuponi zinazopatika katika magazeti hayo.

“Zimesalia wiki chache kabla ya kufanyika droo kubwa ambayo itakuwa ya mwisho ambapo mshindi ataondoka na nyumba ya kisasa. Hatufanyi kwa kubahatisha, tupo katika serikali makini bahati nasibu hii inaendeshwa na watu makini chini ya bodi ya michezo ya kubahatisha.

“Siku ya ufunguzi wa bahati nasibu hii, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisimamia zoezi hili na tunatarajia na siku ya mtu kukabidhiwa nyumba pale Salasala (Dar), atakuwepo,” alisema Mwaipaja.

Katika droo hiyo ndogo, washindi wengine walioshinda na kukabidhiwa zawadi zao ni Marian Mwakale aliyejishindia bed sheet, Richard Mauga aliyejishindia simu ya kisasa ya mkononi ‘smartphone’ pamoja na Aginita Nsemwa aliyejishindia seti ya vyombo vya ndani.

Ndroo kubwa inatarajiwa kuchezeshwa mwezi ujao ambapo mshindi atazawadiwa nyumba ya kisasa yenye samani zake iliyopo Salasala jijini Dar.

(PICHA NA SALUM MAGANGA/STORI NA ANDREW CARLOS-GPL)

Leave A Reply