The House of Favourite Newspapers

Shinda Nyumba, Makonda Mgeni Rasmi

0

Shinda Nyumba na Global (6)Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

Makala: OJUKU ABRAHAM

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amethibitishwa kuwa atakuwa mgeni rasmi katika droo ya mwisho ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba itakayofanyika Alhamis hii katika Viwanja vya Mbagala Zakhem.

Nyumba-11Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, Makonda atashuhudia mshindi wa bahati nasibu hiyo ya nyumba yenye thamani ya mamilioni ya shilingi iliyojengwa maeneo ya Salasala nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Nyumba-8

Nyumba hii ni ile itakayotolewa na Global Publishers kwa mmoja kati ya mamilioni ya wasomaji wake, ambao kwa kipindi cha miezi sita iliyopita, walikuwa wakikata kuponi kupitia magazeti yake ya Championi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Risasi, Amani na Uwazi.

Wengi wamekuwa kama wasioamini kwamba jambo hili litatokea, lakini sasa huenda nyoyo zao zikaondoka wasiwasi, kwani mtu mkubwa kama mkuu wa mkoa, hawezi kwenda kwenye tukio ambalo ni ‘magumashi’.

Nyumba-3Kwa maana hiyo, wale ambao walikuwa na wasiwasi na sasa umeondoka, bado hawajachelewa kupata kuponi zao kupitia magazeti hayo yanayouzwa kwa shilingi mia tano tu (isipokuwa Ijumaa linalouzwa kwa shilingi elfu moja). Mia tano yako leo, inaweza kukufanya ukawa mmiliki wa nyumba kubwa ya thamani hapo Alhamisi.

Itakumbukwa kuwa kabla ya droo hiyo kubwa, droo zingine ndogo zilikwishafanyika kama mara nne hivi katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam, ambapo watu walijishindia zawadi kemkemu, zikiwemo pikipiki, tv flat screen, dinner set na zingine.

Nyumba-2Kitu kimoja kizuri kwenye nyumba hii ya mamilioni ya shilingi ni kwamba, mshindi atakuta samani ndani yake, tena za kisasa kabisa ambazo zitamfanya kutogharamika tena kwa ajili ya fenicha mpya ndani ya mjengo wake.

Nyumba-5Wakati tukihesabu siku kuelekea Alhamisi, nazidi kuwasisitizia wasomaji kuwa hadi mtu atakayenunua gazeti litakalotoka siku moja kabla ya bahati nasibu hiyo, anayo nafasi ya kushinda zawadi hii kubwa ambayo ni ya kihistoria katika Tanzania kuwahi kutolewa na kampuni ya magazeti.

Nyumba-4Hii ni kwa sababu kuponi zote zitakazofikishwa katika ofisi za mawakala wa Global Publishers popote Tanzania, zitatumwa makao makuu tayari kujumuishwa na zingine kwa ajili ya droo hiyo kubwa.

Hivyo msomaji hatakiwi kuacha kununua magazeti kwa sababu ya kuhofia kuchelewa au pengine kuponi yake kutowahi kufika eneo la tukio kwa wakati.

Leave A Reply