Alisema vyama haviwezi kukaa kimya mpaka mwaka 2020 wakati kazi yao ni kukutana na wananchi.
“Tunamshauri Rais Magufuli aache kutawala nchi kwa woga na ubabe … afuate misingi ya Katiba na sheria, na kuwaongoza Watanzania badala ya kuwatawala,” alisema Mabina.
“Hatuwezi kuendelea kama tutashindwa kukaa na wenzetu ili kujifunza mambo ya maendeleo,” alisema.
Mwita alidai kuwa huo ni mpango wa Serikali kudhoofidha halmashauri zinazoongozwa na upinzani ili wasiweze kufanya mambo makubwa ambayo hayajawahi kufanywa na CCM.
Alisema yeye pia alizuiliwa kwenda Marekani akiwa mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii.
Ushauri mwingine ulitolewa na mwenyekiti wa Kanda ya Ilala, Dk Makongoro Mahanga ambaye alimtaka Rais kufuata Katiba kwa sababu aliapa kuilinda na kuitetea kwa masilahi ya Taifa.