The House of Favourite Newspapers

‘Shinda Nyumba’ yatikisa Vikindu-Mkuranga

0

1.Sujkuru

Shukuru Chamu (katikati) akielekezwa na Ofisa Masoko wa Global,Yohana Mkanda namna ya kujaza kuponi yake kushiriki bahati nasibu ya Shinda Nyumba.

Msomaji wa Uwazi aitwaye Rashidi (kulia) akielekezwa namna ya kujaza kuponi.

Jimmy Bulegea (kushoto) akijaza kuponi yake kushiriki bahati nasibu hiyo.

Msomaji wa Uwazi akiweka kuponi yake katika ndoo maalum ya bahati nasibu eneo la Vikindu-Mkuranga.

Abdallah Puga akiweka kuponi yake kushiriki droo kubwa inayotarajiwa kuchezeshwa mwishoni mwa mwezi huu.

 

ZIKIWA zimebaki siku 23 kuchezeshwa droo kubwa ya bahati nasibu ya Shinda Nyumba na mshindi wa nyumba kupatikana,  leo promosheni hiyo inayoendelea ilionekana kuwatikisa vilivyo wakazi wa Vikindu- Mkuranga baada ya kujitokeza kwenye gari la matangazo kuchangamkia gazeti la Uwazi na kushiriki kujaza kuponi ya bahati nasibu hiyo ambayo  inaendeshwa na Kampuni ya Global Publishers wachapishaji wa magazeti ya Champuioni, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Ijumaa Wikienda.

Maofisa Masoko wa Global Publishers,Yohana Mkanda na Jimmy Haroub waliwafikia wasomaji katika mitaa mbalimbali ya maeneo ya Vikindu ambapo waligawa zawadi za kofia zenye nembo iliyoandikwa ‘Shinda Nyumba’ baada ya kununua gazeti la Uwazi.

Mkanda alisema: “ Siku zimebaki 23 wakazi wa Vikindu changamkieni fursa hiyo na mshindi wa nyumba anaweza kuwa miongoni mwenu, hivyo nunueni magazeti ya Global mengi na mjaze kuponi ili kujiongezea nafasi ya kushinda.”

 

NA DENIS MTIMA/GPL

 

 

 

Leave A Reply