The House of Favourite Newspapers

Etihad Yashinda Tuzo ya Heshima ya Adam Smith

0

Adam Smith Awards

Kutoka kushoto ni Naibu wa Fedha Mkuu wa Shirika la Ndege la Etihad, Adam Boukadida, Mkuu wa Idara ya Fedha wa Mashirikia ya Etihad, Ricky Thirion wakiwa kwenye kupokea tuzo za Uhasibu za Adam Smith jijini London hivi karibuni.

Shirika la Ndege la Etihad limeibuka mshindi katika tuzo za Treasury Today Adam Smith jijini London, Uingereza kutokana na ubora na ufanisi mkubwa kwenye masuala ya kifedha.

Idara ya Fedha ya Shirika la Ndege la Etihad imenyakua tuzo hiyo ya juu kwa kuwa mshindi wa kwanza kwenye uongozi bora Idara ya Fedha kwa kuwa mshindi wa jumla. Pia, imeshinda tuzo kwa utoaji bora wa huduma za kifedha na utawala wa fedha.

Kushinda tuzo ya jumla katika ushindani huo wa kimataifa, kumetokana na idara ya fedha ya Shirika la Ndege la Etihad kutambuliwa kutokana na ubunifu wake katika teknolojia na kuwapo kwa mikakati endelevu ambayo imewezesha mchango mkubwa kwenye sekta ya anga.

Akitangaza kwenye Ukumbi wa Gala, jijini London, Gibson Hall, tuzo za Etihad zilipokelewa na Mkuu wa Idara ya Fedha wa Shirika la Ndege la Etihad na msaidizi wake Adam Boukadida.

Rais na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Etihad alisema, “Ubunifu ndiyo msingi wa yale tunayoyafanya kwenye shirika letu. Tuzo hizi ni uthibithisho kwa kazi nzuri tunayoifanya kwenye uongozi masuala ya fedha. Mikakati yetu ipo wazi na ndiyo inayotuwezesha kufanya biashara kwa kisasa inayozingatia ukuaji na uwekezaji zaidi kwenye sekta ya anga ulimwenguni kote. Ushirikiano wetu umetunawezesha kufanya mambo makubwa miongoni mwa yale tuliyonayo ikiwamo, kushirikiana katika kuimarisha mapato, kupunguza gharama za uendeshaji na kuanzisha biashara mpya inayovutia.

Mkuu wa Idara ya Fedha wa mashirika ya Etihad alisema, “Utendaji wa wafanyakazi wetu kwa mwaka huu umetambulika. Tuzo hizi za juu hususani tuzo ya uongozi wa fedha, hakika tulishathili. Mafanikio tuliyopata ni chachu kwa mashirika yaliyopo chini ya Etihad kwa kuweka mipango mizuri zaidi katika ukuaji na uwekezaji.”

Mwanzilishi wa tuzo hizo katika kampuni ya Treasury Today Group, Angela Berry alisema, “Tuzo za Adam Smith huangazia mafanikio yaliyofikiwa katika shirika kwenye masuala ya fedha. Tunaipongeza Shirika la Ndege Etihad kwa kupata tuzo nyingi kwa mwaka huu.”

Tuzo ya Ubora Utawala wa Fedha ilitolewa kutambua Shirika la Ndege la Etihad kutokana na kuwekeza mtaji wa dola 700 mwaka jana mpaka mwezi Septemba.
Ilionekana kama ni mpango wa mara ya kwanza kwenye ushirikiano kifedha katika sekta ya anga, fedha hizo zililenga kupanua maeneo ya uwekezaj ikwenye mashirika ya Etihad. Dola milioni 500 zaidi, zilitolewa katika awamu ya pili iliyoisha mwezi uliopita kwa kuzingatia soko la fedha jambo lililoimarisha Shirika la Ndege la Etihad na washirika wake.

Katika utekelezaji kwenye kukuza mtaji maeneo mbalimbali ilipowekeza ulimwenguni, ilianzisha upunguzaji gharama za uendeshaji jambo lililowezesha shirika la ndege la Etihad kumudu kulisimamia shughuli zake, upatikanaji wa taarifa sahihi za fedha, jambo ambalo limepelekea kupata tuzo ya ubora kwenye usimamizi wa fedha. Jambo hilo ndilo lililotuwezesha kuimarika kiuchumi, kuongeza ufanisi wa uendasheaji, kuongezeka mapato na kukabiliana na utatuzi wa haraka kwenye mahitaji yanayoongezeka kwenye soko la usafiri wa anga ulimwenguni.

TAARIFA ZAIDI

Tuzo zingine ilizopata Idara ya Fedha ya Shirika la Ndege Etihad za hivi karibuni
– Emerging Europe Middle East and Africa Bond of the Year from International Financing Review (IFR)

– Debt Financing Deal of the Year Middle East from Global Transport Finance

– Air Finance Journal’s Innovative Deal of the Year.

– Large Treasury Team of the Year – Association of Corporate Treasurers Middle East (ACTME)

– Treasury Innovation Award – Treasury Management International (TMI)

– Corporate Finance Deal of the Year – Association of Corporate Treasurers’ Middle East (ACTME)

KUHUSU SHIRIKA LA ETIHAD
Shirika la Usafiri wa Anga la Etihad linafanya shughuli zake ulimwenguni kote likifanya biashara kupitia mashirika yake manne ambayo ni; Shirika la Ndege la Etihad, The National Airline of The United Arab Emirates, Etihad Engineering, Hala Group na Airline Equity Partners.
Shirika limewekeza kwenye mashirika saba; : Airberlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Jet Airways, Virgin Australia na Swiss-based Darwin Airline, inayofanya chini ya Etihad.

Kwa maelezo zaidi tembelea: www.etihad.com

Leave A Reply