Shirika la Ndege la Rwandair Lamwaga Zawadi Kwa Wateja, Wadau Wa Tanzania
Shirika la Ndege la Rwanda, Rwandair @flyrwandair hapo jana, Septemba 29, 2023 lilikutana na wateja na wadau wake wa nchini Tanzania katika ‘corporate event’ iliyofanyika katika Hoteli ya Johari Rottana jijini Dar es Salaam nakutoa zawadi kemkemu.
Katika tukio hilo, shirika hilo limewashukuru wateja wake wa nchini Tanzania kwa kuliamini na kusafiri kwa ndege zake ambapo shirika hilo limewahakikishia wateja wake kwamba litaendelea kuimarisha safari zake hapa nchini.
Akizungumza katika event hiyo, Meneja Biashara wa Rwandair, Andrew Best Owie amesema shirika hilo litaendelea kutoa huduma bora na za kuridhisha kwa wateja wake waliopo nchini Tanzania na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda.