

Mkurugenzi Mtendaji wa Lake Energies, Abdirahman Ahmed, akimkabidhi Ayne Magome zawadi ya mtungi wa gesi pamoja na kadi ya kujaza mafuta yenye thamani ya shilingi laki 5/- atakayotumia kujaza mafuta katika vituo vya kampuni ya Lake Energies baada ya kuibuka mshindi wa kwanza upande wa wanawake kwenye mashindano ya NCBA Gofu series yaliofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam jana ambapo kampuni hiyo ilikuwa sehemu ya wadhamini wa mashindano hayo.