The House of Favourite Newspapers

SHOGA: Kubana Ziachie Nguo na Nywele!

0

NAJUA kabla sijaanza na salamu utaanza kujiuliza MC Sophia leo kulikoni tuache kubana! Mara ohhh kubana tuziachie nguo na nywele, heee heeeiyaaaa nicheke miye niongeze siku za kuishi!

Shoga kwa hali mi mzima kama ulivyoniacha, leo nisingependa kuongea saaana tuelekee moja kwa moja kwenye kile kilichonikutanisha mi’ na we’ hapa! Shoga nina imani wengi tunajua baada ya kuandaa chakula na kuanza kula kuna kitu muhimu sana ambacho wengi huwa tunakisahau, naona macho yashakutoka kutaka kujua mnasahau nini!

Jamani uhuru ndani ya mapenzi ili wote mfurahie chakula chenu. Najua unauliza uhuru gani huo? Shoga nawe, utakuwa unajiuliza kila kitu ati!

Basi mwenzako katika pitapita yangu, nimepata malalamiko mengi kutoka kwa wanawake ambao siku zote hufanywa chombo cha starehe na kunyimwa uhuru wa kuzungumza wakati wa mchezo, hufikia hatua hata kama amechoka anaogopa kukaripiwa, hata kuambiwa huenda mchana amemhujumu kwa kutembea na mtu mwingine, Ooh! Hapana haiendi hivyo!

Kwanza lazima ujue safari ya mahaba kama siyo mahabuba inataka nini. Safari ya mapenzi si ugomvi au raha za upande mmoja, unapojisikia unatakiwa utimiziwe hata kama mwenzio anaumwa.

Hii hufanya hata mwanamke apoteze hamu ya mapenzi, kila akuonapo, hata mnapokuwa kwenye dimbwi la mahaba anakuwepokuwepo tu, si kulifurahia bali kutimiza wajibu kwa mumewe au mpenziwe, au siyo shoga!

Kama ulikuwa hujui jua sasa, mapenzi ni upendo, furaha, tulizo la moyo, kato la kiu ya mwili, upo? Mapenzi ni raha ya pande mbili, mapenzi ni kuoneana huruma, ni kuona mwenzio akiondokewa na mawazo na majonzi. Mfanye mwenzako alifurahie lako, alikumbuke uwapo mbali, heee heeeiyaaaa hilo nalo neeeenooo!

Mpe uhuru bibi weee ili akupe penzi kutoka chini ya uvungu wa moyo wake, mwache alie kilio cha furaha siyo kile cha maumivu, wewe na mpenzio kila mmoja ana uhuru wa kufanya atakavyo katika mwili wa mwenzie bila kulazimishana bali kwa kuridhiana, kitu kinachowafanya kila mmoja ajisikie raha na furaha!

Kila kiumbe kina udhaifu wake mnapokuwa kwenye sita kwa sita, hasa wanawake kila mmoja ana namna yake ya kujisikia na kuonesha alivyoguswa sehemu zake, wapo wanaolia utafi kiri wameonewa, maskini kumbe raha zimemzidi, wengine huongea kama wamemeza flash ya maneno, wengine utafi kiri si muda mrefu watakufia kwenye kilinge, pumzi zinawatoka kama wagonjwa wa pumu!

Yote hayo ni kutokana na kuwa huru na kuweza kufanya alichonacho bila uwoga. Ifi ke hatua wanaume tubadilike, Oooh! Nimekumbuka kuna mtu amenitonya eti wanaume wengine huwa wakali kwa kuwa mambo mengi ya mahaba hawayajui, looo!

Lakini kama tupo pamoja toka mwanzo nina imani sasa mwanaume wa aina hiyo ataweza kumfurahisha mpenzi wake bila ngumi wala lugha kali.

Hakuna aliyezaliwa akijua, wote tumejifunza kupitia njia hizi au kuuliza kwa wenzetu, usione aibu kuuliza kwa mwenzio, nina imani kama anajua hawezi kuwa mchoyo atakupa elimu hii kwani ni ya bure shoga wajanja wanakwambia kubana ziachie nguo na nywele, sasa wee bana weee, ona aibu uone utaishije mjini hapa!

Hata wewe una uhuru wa kumpa mwenzio, naye ajikute siku moja chozi limemtoka kwa raha za ajabu ambazo hajawahi kuzipata tangu aingie kilingeni. Nina imani nimeeleweka, tukutane wiki ijayo kwa mada mpya.

Mapenzi & Maisha (Chumbani Zaidi)

Leave A Reply