The House of Favourite Newspapers

Shoga; usilie mumeo kukusaliti, jichunguze!

0

Couple-in-BedKabla sijaanza mada yangu ya leo, napenda kuwafahamisha jinsi nilivyoumizwa na kifo cha mfanyakazi mwenzetu aliyekuwa mwandishi mahiri wa habari za uchunguzi, Makongoro Oging’ aliyefariki dunia juzi Jumapili.

Hakika kampuni yetu ya Global imepata pigo kubwa ambalo nashindwa namna ya kulielezea, kikubwa sinabudi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwani kazi yake haina makosa.

Baada ya kusema hayo, narejea kwenye jambo ambalo nimependa kuzungumza nawe leo linalowahusu baadhi ya wenzetu wanaoishia kulalamika au kulia kufuatia kusalitiwa na waume zao.

Shoga,hakuna kitu kinachoumiza kama kusalitiwa na mumeo unayempenda kwa dhati, hakika maumivu yake hayana kipimo.

Inapotokea mumeo kaamua kukusaliti ukiwa mwanamke makini unatakiwa kukaa chini na kujiuliza kwa nini ameamua kuchepuka badala ya kulalamika.

Nasema hivyo kwa sababu kuna wanaume huamua kutoka nje ya ndoa baada ya kukerwa na mambo f’lani kutoka kwa wake zao,mfano gubu, uchafu, uongo, kutoa penzi kwa masharti, wivu uliopitiliza, kutojali nk.

Inawezakuwa moja au mawili ya hayo niliyoyataja ndiyo sababu ya mumeo kuamua kukusaliti, ukijichunguza na kuyabaini jirekebishe.

Shoga, kama kweli mumeo anakupenda kwa dhati siyo rahisi kukusaliti bila sababu, japo wapo wengine husumbuliwa na tamaa zao tu!

Kama nilivyokuambia hapo juu, ukiona mumeo ameanza kubadilika, anachelewa kurudi nyumbani, akija hali chakula ulichomwandalia au siku nyingine analala nje jua anachepuka hivyo usilalamike wala kulia, jichunguze.

Wapo wanaume ambao ni wepesi kuwaambia wake zao kasoro zao lakini wasipoona mabadiliko hutafuta nyumba ndogo,     hivyo kuwa makini kwani usipochunga mzigo wako wajanja watauiba. Bye!

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: Global TV Online

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE:@shigongotz

Leave A Reply