The House of Favourite Newspapers

Shule za St. MARY’S Zatangaza Ofa Msimu wa Masomo 2020

0

KWA wazazi, inapofika Desemba kuelekea Januari kila mwaka, huwa ni kipindi kigumu sana! Ugumu wake ni majukumu yaliyopo mbele yao kwa sababu Januari ndiyo kipindi ambacho wanafunzi wanaenda shule, wengine wanaenda kuanza na wengine wanaendelea na masomo yao.

 

 

Mtihani ambao huwasumbua wazazi wao, ni kuwatafutia watoto wao shule nzuri, wanakoweza kupata elimu bora lakini kwa ada nafuu!

 

Kwa miaka mingi, shule za St Mary’s zimekuwa suluhu ya changamoto wanazokutana nazo wazazi hasa katika kipindi kama hiki cha maandalizi ya msimu mpya wa masomo.

 

 

Kama ulikuwa hujui, Shule za St Mary’s ndiyo mama wa shule zinazofundisha kwa kufuata mitaala ya Kiingereza au English Medium hapa nchini na ambazo wazazi wengi hata wenye kipato cha kawaida lakini wanaojali ubora wa elimu, huwapeleka watoto wao.

 

 

Shule za St. Mary’s ndizo zilikuwa shule za mwanzomwanzo kabisa nchini kufundisha kwa kufuata mtaala wa Kiingereza, zikiwa zimeanza kuwahudumia Watanzania tangu mwaka 1998 na kwa miaka mingi zimeendelea kufanya vizuri kwenye tasnia ya elimu na kufaulisha watoto wengi ambao wamekuwa hazina kubwa kwa taifa.

 

Wengi ni wahitimu wa vyuo vikuu, wengi wameajiriwa au kujiajiri kwa mafanikio makubwa! Hiyo yote ni kwa sababu ya msingi imara ambao waliupata kutoka Shule za St. Mary’s.

 

 

Habari njema zaidi ni kwamba shule hizo zilizoenea katika maeneo mbalimbali nchini, katika msimu huu wa kuelekea msimu mpya wa masomo wa 2020, zinatoa ofa kubwa kwa wanafunzi wenye vipaji maalum, kujiunga na shule zao kwa punguzo la ada.

 

 

Kama wewe ni mzazi na una uhakika mwanao ana kipaji cha kitaaluma, changamkia ofa hii kwa kwenda katika shule yoyote ya St. Marys iliyo karibu nawe, mwanao atapimwa uwezo wake wa kitaaluma na akifuzu vigezo, basi utapata ofa ya punguzo kubwa la ada!

 

 

 

Shule za St. Mary’s zimesambaa karibu nchi nzima; kuna St. Mary’s ya Tabata, St. Mary’s ya Mbezi Beach na Mbagala zote za jijini Dar es Salaam, St. Mary’s Mbeya, St. Mary’s Dodoma na St. Mary’s Ifakara na St. Mary’s Kihonda zote za Morogoro huku malengo yakiwa ni kuwa na shule katika mikoa yote ya Tanzania.

 

 

Pia zipo Shule za Kenton na East Africa International School ambazo nazo pia zipo chini ya St. Mary’s, zote zikiwa zinafundisha kwa kufuata mtaala wa Kiingereza na kutoa wanafunzi bora kabisa ambao wamekuwa wakipata mafanikio makubwa kwenye elimu za juu ndani na nje ya nchi.

 

“Ushahidi wa ubora wa elimu inayotolewa katika shule zetu ni matokeo ya mitihani ya kitaifa ambapo mara kwa mara tumekuwa tukiibuka vinara katika ngazi za wilaya na mikoa, huku tukishika nafasi nzuri kitaifa,” amekaririwa Rose Rwakatare, mmoja kati ya wakurugenzi wa shule za St. Mary’s na kuongeza:

“Shule zetu zina mazingira bora kabisa ya kujifunzia, walimu wazoefu, maabara za kisasa, maktaba zenye vitabu vya ziada na kiada vya kutosha huku pia masomo ya kompyuta na lugha ya Kifaransa yakifundishwa kwa vitendo hivyo kumjengea mtoto uwezo mkubwa wa kuendana na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia.”

 

Rwakatare ameongeza kwamba ili kuwapunguzia wazazi changamoto za kiuchumi, kuna utaratibu maalum wa mzazi kulipa karo kidogokidogo, huku pia kukiwa na huduma nzuri za chakula na usafiri kwa watoto wote.

 

Namna ya kuwasiliana nao, unaweza kupiga namba za simu zifuatazo kulingana na shule unayoitaka ambayo itakuwa rahisi kwako kumpeleka mwanao:

St. Mary’s Mbeya (0713435776), St. Mary’s Dodoma (0718088834), St. Mary’s Morogoro (0713212911), St. Mary’s Mbezi Beach Dar es Salaam (0654994193), St. Mary’s Mbagala Dar es Salaam (0713427641), St. Mary’s Tabata (0754428183) na East Africa International School (0713217898).

Pia unaweza kuwatembelea kwenye mtandao wa Instagram kwa anuani ya @st.marys_schooltz.

“Ushahidi wa ubora wa elimu inayotolewa katika shule zetu ni matokeo ya mitihani ya kitaifa ambapo mara kwa mara tumekuwa tukiibuka vinara

 

 

Leave A Reply