The House of Favourite Newspapers

Siasa Yamponza nyota wa Bafana Bafana, Tenoho Mokoena

0

Klabu ya Al Ahly ya Misri imeahirisha mpango wake wa kumpa nafasi ya majaribio nyota wa Bafana Bafana, Teboho Mokoena.

Katika taarifa yao ya Feburuari 15, 2024  Al Ahly wamesema wamefikia uamuzi huo kutokana na misimamo ya kisiasa ya mchezaji huyo.

Hivi karibuni wakati Bafana Bafana wakirejea nyumbani kutoka Ivory Coast kwenye AFCON ambako walimaliza katika nafasi ya tatu, Mokoena alielezea mapenzi yake kwa Julius Malema, Rais wa chama cha upinzani cha EFF cha Afrika Kusini.

Katika taarifa yao, Al Ahly wamesema wamesikitishwa na Mokoena kumuunga mkono Malema ambaye anahubiri chuki yakiwemo mauaji dhidi ya wazungu wa Afrika Kusini.

Majaribio ya Mokoena klabuni Al Ahly yalipangwa kufanyika mwezi ujao lakini sasa ni hadi itakapoamriwa vinginevyo.

MBUNGE ALIYEFATA MONDULI BAADA YA LOWASSA – DC KALANGA AFICHUA SIRI YA KUACHIWA JIMBO NA LOWASSA…

Leave A Reply