The House of Favourite Newspapers

Rais Mstaafu Kikwete Aongoza mazishi ya aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Ibrahim Msabaha

0

Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Jumatano ameungana na ndugu, jamaa na marafiki kwenye mazishi ya aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Ibrahim Msabaha (72) aliyefariki dunia Jumanne, Februari 13, 2024.

Mazishi hayo yamefanyika nyumbani kwa marehemu huko Kibaha, mkoa wa Pwani.

Hayati Dkt. Msabaha alifariki dunia akiwa njiani akipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya hali yake kubadilika ghafla ikiwa ni siku chache tangu atoke Hospitali hapo alikokuwa amelazwa.

Aidha, Dkt. Msabaha amewahi kuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Kibaha, mkoani Pwani kupitia Chama cha Mapinduzi

 

MBUNGE ALIYEFATA MONDULI BAADA YA LOWASSA – DC KALANGA AFICHUA SIRI YA KUACHIWA JIMBO NA LOWASSA…

Leave A Reply