Sibomana Aweka Rekodi Mpya Caf

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Patrick Sibomana juzi aliweka rekodi mpya kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika ambayo inasimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf).

 

Mshambuliaji huyo ambaye aliichezea Yanga mchezo wake wa kimataifa kwa kwanza kuanzia alipojiunga nayo akitokea Mukura ya Rwanda, amekuwa staa kwenye timu hiyo kuanzia alipojiunga nayo.

 

Sibomana aliifungia Yanga bao lake wakati ilipotoka sare ya bao 1-1 na Township Rollers ya Botswana kwenye mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

Hata hivyo, Sibomana ambaye hadi sasa kwenye mchezo huo mmoja wa kimataifa na michezo ya kiraļ¬ ki aliyocheza ameshafunga mabao nane aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kwa msimu huu kufunga bao la penalti na wakati huohuo kukosa penalti kwenye Klabu Bingwa.

 

Katika michezo yote ya awali iliyopigwa kuanzia Ijumaa hadi Jumapili, hakuna mchezaji ambaye aliweza kufanya jambo hilo la kufunga penalti na kwenye mchezo huohuo kukosa penalti. Hata hivyo, mbali na huyo pia Yanga iliweka rekodi ya kupata penalti mbili kwenye mchezo mmoja kati ya hiyo yote ya kimataifa iliyopigwa juzi.


Loading...

Toa comment